Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty InternationalPicha: Pond5 Images/IMAGO
Shirika la Amnesty International limetoa taarifa likieleza kuwa mamlaka za Tanzania zimeongeza ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa, waandishi wa habari, asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu.
Shirika hilo limesema yote hayo yanafanyika kwa lengo la kueneza hofu na kudhibiti ushiriki wa raia kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025. Taarifa hiyo inasema kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan , matumaini ya mageuzi yameyeyuka, huku ukandamizaji ukiendelea kwa njia ya mashambulizi, kukamatwa kiholela, mauaji ya kiholela na watu kutoweka kwa nguvu bila yeyote kuwajibishwa.
Amnesty pia imebaini ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo wa haki za binadamu, ikiwemo mateso, unyanyasaji, na mauaji ya kiholela ya viongozi wa upinzani na wanaharakati.
Shirika hilo linazitaka mamlaka za Tanzania kusitisha kampeni ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani, kufuta mara moja mashtaka ya uongo na yenye nia ya kisiasa dhidi ya wote waliokamatwa kwa sababu ya maoni yao ya kisiasa au kidini akiwemo kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.