Vifaa vitumiwavyo na watu wengi.


Katika mada hii, nitakuonyesha au kufundisha kujua vitu vitumiwavyo sana na watu wengi. Watu wengi hawajaamaua kutambua kuwa kuna vitu huwa vinatumika mara nyingi sana na watu wengi mno, na wewe unakuwa ni mmoja wa hao watu unaotumia vitu hivyo. Lengo ni kujua vifaa ambavyo hutumiwa na watu wengi, na jinsi ya kuchukua tahadhari ya jinsi ya kuvitumia, au kanuni za muhimu za kuzingatia katika kuvitumia vifaa malaya.
Nimetumia neno “Malaya” Nikiwa maana kuwa, ni kitu kisichochangua ni yupi wa kukitumia au kifaaa cha wote.
VIFAA MALAYA.

  1. Vijiko/uma. Vijiko na uma, vitumiwavyo na mtu zaidi ya mmoja, haswa vikiwa hotelini, vinakadiriwa kutumiwa na watu wasiopungua 30 kwa mwezi, au watu 20 kwa siku. Inashauriwa vijiko vioshwe kwa maji safi na sabuni, lakini ikiwa ni hotelini basi vijiko vichemshwe kwenye maji ya moto, na mteja apewe kijiko kutoka katika maji ya moto. Kwani midomo mingi sana imetumia kijiko hicho.
  2. Vikombe vya chai/kahawa, na glasi za juisi hotelini au sehemu za biashara.
    Inakadiriwa kikombe kimoja au glasi moja, inaweza kutumiwa na watu zaidi ya 10 hadi 50 kwa siku. Hivyo unaona kiasi gani kikombe kimoja kilivyotumika na midomo mingi?
    Inashauriwa vikombe vioshwe na maji safi yanayotiririka ya bomba, na sabuni, ikiwezekana vitumbukizwe kwenye maji moto na kutolewa kabla ya kutumiwa na mtu mwingine. Pia usitumie kikombe chenye ufa au mapengo.
  3. Sahani za chakula. Ni miongoni mwa viombo malaya vitumikavyo na watu wengi, ushauri, vioshwe na maji safi na sabuni, na ikiwezekana na maji yaliyochemka(Yaani, baada ya kuviosha, kisha unavitumbukiza katika maji ya moto).
  4. Kofia za pikipiki(bodaboda) Ni miongoni mwa vitu malaya, vitumikavyo na watu wengi kwa siku moja, inakadiriwa kutumiwa na watu kumi hadi 50. Ushauri, Vaa kofia na kitambaa (leso) ndani, au nailoni. Aidha inashauriwa kofia zioshwe na sabuni kila baada ya siku tatu.
  5. Vifaa vya saluni(kunyolea nywele sehemu za biashara) kama vile mashine za kunyolea, taulo au vitambaa vya kufutia, brashi, nk. Vyote ni vifaa malaya, inakadiriwa mashine za kunyolea sehemu ya biashara, inanyoa watu wastani 20 hadi 100 kwa siku moja. Ikiwa na maana hiyo mashine imetumiwa na watu wa aina mbalimbali na wenye matatizo mbalimbali kichwani. Aidha vitambaa hupangusia watu wengi kwa siku, na baadhi ya wanyoaji sio wasafi hawafui vitambaa. Ushauri, penda kunyoa na mashine yako binafsi nyumbani kwako, au unapoenda kunyolewa saluni hakikisha vifaa wanavyovitumia ni safi na salama.
  6. Vyoo vya kulipia(public toilets). Ni vyoo vitumiwavyo na watu wengi mno kwa siku moja, na wenye kila aina ya matatizo. Ushauri, ukikuta maji kwenye pipa au ndoo chooni usiwe mwepesi wa kuyatumia kujisafishia, kwani kuna baadhi ya watumiaji vyoo hivyo huingiza uchafu, kwa mfano kudondoshea mikojo, au mikono yao michafu na wanachota maji kwenye ndoo au pipa na kutumbukiza na uchafu wa mikononi mwao. Aidha unashuriwa kama maji yanatoka katika bomba, basi usitumie maji yaliyo kwenye ndoo au pipa, bali tumia ya bombani moja kwa moja au tumia katarasi maalumu za chooni.
  7. siti/kiti/viti vya kwenye basi, treni, ndege, bodaboda, ofisi kwenye idadi kubwa ya watu wanaopanga foleni kila siku, kiti cha dereva kwa magari yanayoendeshwa na madera zaidi ya mmoja kwa siku. Hivyo huitwa vitu malaya. Kwani hutumiwa au hukaliwa na watu wengi mno kwa siku. Aidha unapoegemea kiti kwa kichwa pia ujue watu wengi wameegemea kwa kichwa kama wewe. Ushauri, chunguza kiti kabla ya kukaa au kukitumia, kama utaona dalili za uchafu chukua tahadhari. Au pia inashauriwa ukisafiri uwe na aina ya kitambaa cha kutandika katika kiti utakachotumia iwapo huridhishwi na usafi wake. Aidha wenye magari ya abiria wanashauriwa kufanya usafi vya kutosha, na kupulizia dawa za kuua wadudu.
  8. Gesti/Nyumba za kulala wageni. Vifaa malaya katika hizi nyumba ni. Taulo, shuka, neti, vyoo, mabafu, magodoro, ndala za gesti, sabuni zilizotumiwa na zaidi ya mtu mmoja, sehemu ya kuwekea sabuni bafuni. Hivi ni vitu malaya, cha kuzingatia na kukagua zaidi ni shuka na taulo, kwani taulo mara kadhaa kuna wateja wachafu hufutia sehemu za siri wakitoka kuoga au hufutia miguu. Ushauri. Ikiwezekana unapo safiri, safari ndefu ya kulala ugenini, uwe na shuka na taulo ndogo kwa akiba, pia uwe makini unapotumia vifaa vingine vya kuchangia, hakikisha usafi wa vifaa hivyo.
  9. Vyoo vya kukaa na vya kukojolea wanaume vya wima(juu). Ni moja ya vyoo malaya, kwani wengi hukaa kwenye vyoo hivi na vinahitaji usafi wa kutosha, na vile vya kusimama, jihadhari kusogea karibu zaidi, isije mikojo ikagoga katika sinki kisha ikakurukia, kwani itarudi na mikojo mingine ya watu kutoka katika sinki na ukahatarisha kupata magonjwa.
  10. Kusalimiana kupitia mikono/midomo. Mikono ni moja ya vitu malaya ambapo mikoni inakazi nyingi sana na inashikana na mikono mingi kwa siku na kupangusa uchafu jasho na kujikuna nk. Hivyo, ni vema utambue kuwa mikono na midogo hufanya kazi zaidi ya moja. Ushauri, uwe na kitambaa cha jasho ujifutie badala ya kutumia mikono, na usile kitu bila kunawa mikono na sabuni kwani inawezekana mikono ya watu uliyoshikana nayo, wengine wameshika uchafu na kukushika wewe.
    MAOMBI KWA AJILI YA AKILI.
    Katika utumishi wangu kama Mchungaji kwa miaka zaidi ya 20, hadi mwaka huu 2018 kitabu hiki kinakufikia, sijawahi kusikia mara nyingi kama kuna maombi ya kuombea akili. Yaani wachungaji au Mashekhe nk. Waitishe mkutano au ibada ya kuombea akili. Au kuwafundisha watu waone umuhimu wa kuombea akili, au kuomba wawe na akili nyingi.
    Sijui inaonekana ni makosa au vipi? Au wanaona kama akili ni dhambi? Sisemi kama hawapo kabisa watu wanaombea au omba ili wawe na akili, bali kama wapo ni wachache sana. Kwa ufupi watu wengi na dini nyingi hazioni/hawaoni umuhimu wa kuomba maombi kwa Mungu ili awape akili au awaongezewe akili zaidi.
    Sijui ni kwa nini tunakosa ujasiri wa kumuomba Mungu atupe akili zaidi wakati maandiko hayajakataza kuomba chochote?. Tunaposoma. Yohana 14:14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Kama maandiko yalishasema tukiomba neno lolote kwa jina lake atalifanya, na hakuna mipaka ya kuomba kwa nini kama tunahisi hatuna uwezo mzuri wa akili tusiombe kwa Mungu atuongezee akili?
    Bila shaka huu ni wakati wako wa kuanza maombi ya kumuomba Mungu akuongezee akili au akupe uwezo mkubwa kiakili. Mathayo 7:7.11. Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
    Kumbe maandiko yapo wazi sana, kuwa, kila aombaye atapewa, na ya kwamba, hakuna baba au mzazi ambaye atapenda kumpa mtoto wake vitu vibaya. Bali wazazi wote hupenda kuwapa watoto wao vitu vizuri. Na kitu kizuri mojawapo ni akili ndio kitu kizuri sana tunapaswa kupewa na Baba yetu wa mbinguni
    ………MWISHO
    Neno la Mwandishi wa Makala. Napenda kuchukua nafasi hii kwa kumshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii adimu sana ya kufundisha katika Gazeti hili, pia naamini kabisa watu wengi mmefaidika sana na makala zangu, nami nafurahi sana kwa kupokea simu zenu kwa muliobahatika kusoma na kuchukua hatua ya kunipigia simu kwa kutoa pongezi, asanteni sana. Pia na ushukuru uongozi wa Gazeti hili kwa kunipatia nafasi hii nasema Mungu awabariki sana. Mwisho nawaalika wasomaji wangu kwa makala yetu mpya inayohusu UCHUMI. Na kwa maelezo zaidi kuhusu mada za makala hii tafuta kitabu cha KUWA NA UWEZO MKUBWA KIAKIL, nilichokiandika.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment