Trump atishia kuiangamiza Hamas ikiwa itakiuka makubaliano

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habariPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amelionya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas kuwa “litaangamizwa” ikiwa litakiuka mpango wa kusitisha vita huko Gaza.

Hata hivyo Trump amesisitiza kuwa anatoa nafasi kwa kundi hilo kuheshimu makubaliano hayo, na ameitoa kauli hiyo wakati akimtuma Jumanne nchini Israel Makamu wake JD Vance ili kuungana na wajumbe wawili wakuu wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner kujadili hali inayoendelea huko Mashariki ya Kati baada ya ghasia za hivi karibuni.

Makubaliano hayo ya kusitisha vita Gaza  yaliyosimamiwa na Trump na yaliyoanza kutekelezwa Oktoba 10, yalikuwa hatarini kuvunjika baada ya wanajeshi wawili wa Israel kuuawa kusini mwa Gaza, na kupelekea Israel kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Hamas na kusababisha vifo vya Wapalestina wapatao 45.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment