Mashujaa Dei 2025: Ruto ataka vijana 100,000 wenye biashara kupewa Sh50, 000 kila mmoja

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

  • Shiriki mitandao ya kijamii:

Rais William Ruto. Picha|Maktaba

RAIS William Ruto amewataka mawaziri wake, makatibu na wahudumu wa serikali kumsaidia kupata vijana 100,000 waliowekeza kwenye biashara ili kupigwa jeki.

Kiongozi wa nchi, akihutubu Jumatatu, Oktoba 20, 2025 wakati wa maadhimisho ya Mashujaa Day, alisema anataka idadi hiyo ya vijana kabla ya mwisho wa mwaka.

“Serikali, kabla ya mwisho wa mwaka huu itapiga jeki vijana 100,000 walio kwenye biashara kila mmoja akabidhiwe Sh50, 000,” Rais aliahidi.

Dkt Ruto alielezea kwamba hatua hiyo ni mojawapo ya ahadi zake 2022, kupiga vijana jeki nchini kujiendeleza kibiashara.

Miezi michache 2022 baada ya kuchukua dhana za uongozi, Rais alizindua mpango wa Hustler Fund – mradi uliolenga kuinua wafanyabiashara.

Fedha hizo za mkopo zikitolewa kwa njia ya simu, baadhi ya waliochukua wameripotiwa kukosa kurejesha.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment