Wahouthi wawashikilia wafanyakazi 20 wa Umoja wa Mataifa

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Wapiganaji waKihouthi wa Yemen wakiwa katika maandamano mjini SanaaPicha: Osamah Yahya/dpa/picture alliance

Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wanawashikilia wafanyakazi wapatao 20 wa Umoja wa Mataifa, baada ya kuvamia kituo kingine cha taasisi hiyo ya kimataifa katika mji mkuu wa Yemen – Sanaa.

Ofisi ya mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini  Yemen , imesema wafanyakazi hao akiwemo mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF nchini Yemen, wanazuiliwa katika kituo kilichopo katika kitongoji cha Hada kusini magharibi mwa mji wa Sanaa.

Umoja wa Mataifa umesema unawasiliana na kundi hilo la waasi pamoja na wadau wengine ili kujaribu kutafutia suluhu tatizo hilo na kurejesha udhibiti kamili wa vituo vyake huko Sanaa.

Waasi wa Kihouthi  wamekuwa wakiwashutumu bila ushahidi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuwa majasusi wa Marekani na Israel, shutuma zinazokanushwa na Umoja wa Mataifa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment