Majambazi waiba vito vya thamani jumba “Le Louvre”, Paris

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Polisi wakiwa mbele ya Jumba la makumbusho la Louvre jijini ParisPicha: Gonzalo Fuentes/REUTERS

Kundi la majambazi wanne limefanikiwa siku ya Jumapili kuiba vito vya thamani isiyokadiriwa katika Jumba la Makumbusho Le Louvre jijini Paris, Ufaransa.

Tukio hilo lilitokea Jumapili majira ya saa tatu asubuhi kwa saa za Ufaransa, ambapo wahalifu hao waliingia katika jumba hilo lililoko katikati ya mji mkuu wa Ufaransa na kuiba vitu kadhaa vya sanaa na vito vyenye thamani kubwa kabla ya kutoroka kwa kutumia pikipiki.

Polisi wa  Ufaransa  wamesema watu hao wanasakwa vikali. Jumba hilo maarufu zaidi duniani limetangaza kufungwa kutokana na hali ya dharura.

“Musée du Louvre” ni Makumbusho maarufu duniani inayotembelewa na watu wengi kutoka kila pembe ya dunia ambapo miongoni mwa mambo mengine, umaarufu wake ni  kutokana na uwepo wa mchoro wa Monalisa uliochorwa na msanii mkubwa duniani Leornado Da Vinci.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment