Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Chama cha Demokrasia na Maendelea, CHADEMA kimesema kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,John Heche amewekwa kizuizini.
CHADEMA kimedai kuwa Heche amekamatwa hii lao majira ya mchana mkoani Mara kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya huko Isibania One Stop Border alipokuwa anataka kuingia Kenya.
”Ikumbukwe kuwa jana tulitoa taarifa kuwa Mh. Heche atakwenda nchini Kenya kukiwakilisha chama kwenye shughuli za mazishi ya mwanasiasa nguli wa Kenya,Raila Amolo Odinga.” Ilieleza taarifa hiyo.
Pamoja na kumuweka kizuizini taarifa hiyo inasema kuwa, Mamlaka ya Uhamiaji Tanzania imemnyang’anya hati yake ya kusafiria bila kueleza kwanini wamechukua uamuzi huo.
”Kumzuia Mh. Heche kwenda kuwapa pole Wakenya ni kuwanyima raia wa nchi hiyo haki yao ya kufarijiwa wanapofikwa na majanga mbalimbali ikiwemo msiba”.
”Tunaitaka serikali imuachie mara moja Heche na iache kuwanyanyasa viongozi wa chama chake, kuwapora haki yao ya kutoka nje na kuingia ndani” Ilihitimisha taarifa yake.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.