Buriani Raila Odinga: Shughuli ya kumuaga ‘Baba’ inaendelea Kisumu

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Raila Odinga aliyefariki nchini India alipokuwa akipokea matibabu alikuwa kinara wa siasa za upinzani nchini Kenya kwa zaidi ya miongo mitatu.

Mwili wa Raila unasafirishwa kwa helikopta hadi Bondo

Ndege

Mwili wa Raila Odinga unasafirishwa hadi mjini Bondo kwa helikopta ya kijeshi kwa sasa baada ya shughuli yab kutazama mwili kukamilika mjini Kisumu.

Hatua ya kusafirisha mwili kwa ndege imechukuliwa na kamati ya mazishi ya Odinga kwa ajili ya kuzuia umati mkubw auliopo Kisumu kuchelewsha mwili huo kufika nyumbani kwake OPODA FARM kwa wakati unaofaa.

Kabla ya kuondoka, mapadri wa kijeshi walisimama na kuomba duah fupi wakati jeneza lilipokuwa linafungwa na maafiswa wa jeshi la Kenya. Kikosi maalum cha makomando wa jeshi la KDF lilizingira mwili na kuulinda vilivyo wakati jeneza lilipokuwa linatengezwa tena kwa ajili ya kuwekewa bendera ya taifa kabla ya kuingizwa kwenye ndege hiyo aina ya helikopta.

Tangu kuwasili Kisumu kwa ndege ya kijeshi aina ya SPARTAN, mwili wa Raila haujasafirishwa kwa barabara japo umekuwa ukisafiri hatua fupi tu kwa kuwa uliwekwa kwa ndege aina ya helikopta na kuseafirishwa hadi uwannja wa mamboleo ambao ulijaa mapaema alfajiri.

Mwili huo utapokelewa na mjane wake Ida Odinga aliyeasili nyumbani mapema leo na wanawe wakiongozwa na Raila Odinga Jr aliyeondoka Mamboleo nusu saa kabla ya maiti ya Baban yake kuondoka uwanjani humo.

Mjane wa Raila Odinga, awasihi Wakenya kudumisha amani

Ida Odinga

Mjane wa Raila Odinga , mama Ida Odinga amewataka wakenya wanaokusayika katika uwanja wa michezo wa Jommo Kenyatta Mamboleo na katika mji wa bondo kudumisha amani na kuheshimu hadhi ya Raila aliyeenziwa na wengi kimataifa.

Ida ambaye amewasili katika boma lake la OPODA FARM muda mfupi uliyopita, amewataka wakaazi kutulia na kufuata utaratibu uliwekwa kwa ajili ya kuuona mwili na kutozua vurugu kama ilivyoshuhudiwa katika siku mbili zilizopita.

‘’Nimempoteza mume wangu na mwenza wa miaka mingi, na watoto wangu wamempoteza baba yao. Ndugu zake wamempoteza kaka na vile vile ni mtu aliyeenziwa na wengi duniani. Nimepokea risala nyingi za rambi rambi ambazo ninatarajia kuzisome hapo kesho. Kifo chake ni pigo kubwa kwa sababu ametuacha, hatuna budi kustahamili uchungu. Lakini kwa hilo naomba tumuomboleze kwa heshima na kuhakikisha amani inadumishwa,‘’alisema Bi Odinga.

Matamshi yanakuja saa chache baada ya maafisa wa kuu wa jeshi na polisi kulazimika kusimamisha shughuli ya kutazama mwili hata kabla ya kuanza katika uwanja wa Kasarani siku ya Jumatano ili kudhibiti umati mkubwa uliokuwa unatishia kuwazidi maafisa wa polisi na jeshi waliokuwa wanalinda mwili wa Odinga.

Imebidi Jeshi kuleta kikosi maalum cha makomando kulinda mwili na hata kulinda lango kuu la nyumba yake pale OPODA FARM ili kuzuia utovu wa usalama.

Raila Odinga alitarajiwa kusafirishwa kwa gari hadi nyumbani kwake kama heshima ya jinsi alivyoishi maisha yake na kutangamana na watu, ila sasa serikali imesema kwamba jeneza lake litasafirishwa kwa ndege hadi Bondo ili kuzingatia mipango mingine ya mazishi kwa muda uliowekwa kabla ya ibada ibada maalum itakayodumu yaani VIGIL kuandaliwa.

‘‘Ningetamani sana kwa kaka yangu kusafrishwa kwa barabara na kupewa buriani na watu waliompenda ila sasa wanataka aje kwa ndege, sijapenda hilo ila ndivyo mambo yalivyo kwa sasa,” alisema Ruth Odinga, dada ya Raila Odinga na mbunge wa kaunti ya Kisumu.

Mama Ida awasili nyumbani Bondo tayari kwa masishi ya mumewake

Mjane wa Raila Odinga, Ida Odinga.
Maelezo ya picha,Mjane wa Raila Odinga, Ida Odinga.

Mjane wa Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, Mama Ida Odinga amewasili nyumbani kwake Opoda Farm kwa mara ya kwanza tangu alipoondokewa na mume wake.

Mama Ida amefika nyumbani hapo akiwa na binti yake Rosemary Odinga pamoja na viongozi mbali mbali ambao wamekuja kumfariji anapojiandaa kuupokea mwili wa Odinga ambao kwa sasa unaagwa katika uwanja wa Mamboleo Kisumu.

Baada ya shughuli hiyo kukamilika mwili wa hayati Raila utasafirishwa hadi Bondo ambako utalazwa kabla ya kuzikwa hapo kesho Jumapili.

Shirika la ndege la Kenya Airways latoa salamu za rambirambi ndani ya ndege

.

Shirika la ndege la Kenya Airways limetoa rekodi ya kumuenzi Marehemu Raila Amolo Odinga kwenye ndege ya KQ203 iliyosafirisha mwili wake kutoka India hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Alhamisi asubuhi, Oktoba 16.

Ndege hiyo ya KQ ilibadilishwa jina na kuwa RAO001, herufi za kwanza za jina la Raila na kuhusiana na mchango wake halali katika historia ya nchi.

Imesimuliwa na Kapteni Saviemaria Ondego, heshima hiyo ilifichua jinsi ushawishi wa Waziri Mkuu huyo wa zamani ulivyovuka Kenya na Afrika.

Mabibi na mabwana, huyu ndiye nahodha wenu anayezungumza. Leo, tunatambua msiba mkubwa uliotupata kote nchini Kenya na Afrika.

Kwa niaba ya familia ya Kenya Airways, tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa kuondokewa na Mheshimiwa Raila Odinga. Kiongozi mwenye maono na mwanamajui wa Afrika.

Ushawishi wake unavuka mipaka, na kuwatia moyo wengi kwa kujitolea kwake kwa amani na azma ya kushughulikia changamoto za bara letu.

Viongozi waanza kuwasili nyumbani kwa Raila Odinga Bondo

Raila Odinga

Viongozi wa kitaifa na wale wa majimbo ya magharibi mwa Kenya wanamiminika katika makazi rasmi ya Raila Odinga ya OPODA FARM kuifariji familia inayojiandaa kwa mazishi yake hapo kesho.

Gavana wa Busia Paul Otuoma amefika hapo akiwa amevalia kofia lilotengenezwa na ngozi ya tumbili na akiwa amebeba mkuki akiandamana na kundi watu kutoka Busia.

Kama wageni wengine wengi, viongozi hao wameleta ngombe na vyakula mbali mbali kama kuku, ndizi, mboga, Samaki na mengien mengi kama sadaka ya chakula kitakachoandaliwa kwa wageni watakaohudhuria mazishi ya Raila siku ya Jumapili.

Tangu siku ya Alhamisi, kumekuwa na matambiko ya kitamaduni yanayofahamika kama TERO BURU kwa lugha ya dholuo ambayo yanafayika kumuenzi kiongozi wa hadhi ya juu kama Raila na pia kufukuza pepo mbaya ambazo huenda zimeingia katika boma la laiyefariki.

TEROBURU ni jina la Nyati ambaye ni mnyama anayehofiwa na wengi kwa nguvu zake na uwezo wake kukabiliana na maadui kama vile simba ambao wanamuwinda porini.

Tambiko hizo zitaendelea hadi kesho ambapo Odinga atazikwa na kulingana na mwelekeo wa familia kaburi lake litafunikwa na kuwekwa sanamu ya SIMBA kufanana na kaburi la baba yake Jaramogi Oginga Odinga.

Kabla ya wananchi kuanza kuuaga mwili wake katika uwanja wa Mamboleo mapema leo, kiongozi wa jamii ya Waluo alifanya maombi ya kitamaduni kwa lugha ya Kijaluo ambapo alimuomba Mungu wa jamii ya watu wa RAMOGI kumhifadhi mwana wake pema.

”Mungu wa jamii ya RAMOGI uliyesimama na sisi Wajaluo tulipokuwa safarini kutafuta makao yetu, ulisimama nasi vitani tulipopigania haki zetu na hatimaye ukatupa makazi katika ufuo wa ziwa Victoria. Ulitupa mtoto wa kiume, mkombozi, kiongozi na kwa sasa tumepata pigo kama vile kupigwa na radi ambalo limetikisa wingu na anga na kwa sasa anga linagiza kubwa,’’ alisema kiongozi huyo.

Katika boma la Odinga, aliyekuwa mgombea Urais 2022 Prof George Wajakoya amemtaja Odinga kama ENIGMA, Agwambo ambaye atakumbukwa milele kwa alichokifanya kuipigania Kenya.

Buriani Raila Odinga: Gavana wa Siaya awataka wakazi kuwa watulivu

.

Gavana wa Kaunti ya Siaya Aggrey Orengo ametoa wito kwa wakaazi wa jimbo hilo kudumisha amani wanapojiandaa kwa mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga.

Amesema Mwili wa Odinga utalazwa nyumbani kwake Bondo usiku wa leo lakini watakaopata fursa ya kumuaga itatolewa kwa jamaa zake na wandani wa karibu wa familia yake.

Hapo jana ndugu ya Raila Odinga Seneta Oburu Odinga alielezea kusikitishwa kwake na tukio ambapo waombolezaji walitupiwa vitoa machozi katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

‘’Raila ilirushiwa mabomu ya machozi akiwa hai sitaki atupiwe mabobu ha machozi wakati anapoagwa,’’alisema Oburu.

Maafisa wa usalama wamekuwa na kibarua kigumu wadhibiti idadi kubwa ya waombolezaji waliojitokeza kumuaga Raila katika uwanja wa Kasarini. Watu wawatatu waliiuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Tukio kama hilo pia lilishuhudiwa katika uwaja wa kitaifa wa Nyayo hapo jana wakati wa ibada ya mazishi ya kitaifa ambapo makumi ya watu walijeruhiwa katika mkanyagano.

Buriani Raila Odinga: Shughuli ya kumuaga ‘Baba’ yaendelea Kisumu

Maelfu ya waombolezaji wanaenedelea kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga jijini Kisumu magharibi mwa Kenya.

Baadhi ya wakaazi wa jiji la Kisumu na maeneo yaliyo karibu wanalia kwa huzuni, wakiimba na kupunga mikono kama ishara ya mila ya jamii ya Wajaluo ya kumuaga shujaa aliyefariki.

Wengi hapa wanamtaja Bw Odinga kuwa kiongozi aliyetanguliza masilahi ya taifa, wakati mwingine akihatarisha maisha yake katika harakati za kupigania utawala bora.

Licha ya kufanya kazi na serikali 3 kati ya 4 zilizotangulia nchini Kenya, mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 80 alionekana na wengi kama sura ya siasa za upinzani.

Na huku nchi ikisubiri kumzika Odinga siku ya Jumapili, wengi wanahoji ni nani sasa ataongoza mapambano ya demokrasia na heshima ya utawala wa sheria nchini Kenya.

Maelfu ya waombolezaji wakusanyika Kisumu kutoa heshima zao za mwisho

Waombolezaji

Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika katika jiji la Kisumu kando ya ziwa kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kanya Raila Odinga aliyefariki alipokuwa akipokea matibabu nchini India.

Bw.Odinga alikuwa kinara wa upinzani na aliyejishughulisha na siasa za uchaguzi kwa zaidi ya miongo 3.

Mwili wa Raila Odinga ulikaribishwa kwa nderemo, vifijo na vilio kutoka kwa maelfu ya wafuasi wake katika uwanja huo.

Waomboleaji

Machozi yalimwagika na vijana kwa wazee walipokuwa wakimsherehekea kiongozi huyo ambaye aliwakilisha maslahi yao katika nyanja ya kisiasa ya Kenya kwa karibu miaka 40, anaripoti mwandishi wetu Roncliffe Odit akiwa jijini Kisumu.

Wengi hapa wanamtaja Bw Odinga kuwa kiongozi aliyetanguliza masilahi ya taifa, wakati fulani akihatarisha maisha yake katika harakati za kutafuta utawala bora.

Licha ya kufanya kazi na serikali 3 kati ya 4 zilizotangulia nchini Kenya, mwanasiasa huyo alionekana na wengi kama sura ya siasa za upinzani.

Na huku nchi ikisubiri kumzika Odinga siku ya Jumapili, wengi wanahoji ni nani sasa ataongoza mapambano ya demokrasia na heshima ya utawala wa sheria nchini Kenya.

Katika picha: Mwili wa Raila Odinga ulivyopokewa katika uwanja wa Jomo Kenyatta Kisumu

.
,
.
.
.
.

Obama amuomboleza Raila Odinga

Obama

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama ametaja aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga kama shujaa aliyepigania demokrasia sio tu nyumbani Kenya bali kote barani Afrika.

Katika risala ya rambi rambi kwa Wakenya, Obama alimkumbuka Odinga kama mtoto ambaye baba yake alifungwa na serikali ya mbeberu kwa ajili ya kupigania uhuru wa Kenya mnamo 1952.

‘‘Mara kwa mara nilipokutana naye, nilishuhudia akiweka taifa mbele ya haja zake za kibinafsi. Na kama viongozi wengine duniani alikuwa tayari kufuata mkondo wa kutafuta maridhiano na upatanisho hata baada ya muda ya kukabiliwa na hali ngumu.’ alisema Obama katika ujumbe wake.

Obama ambaye ana asili yake kutoka kaunti ya Siaya alikozaliwa baba yake Hussein Obama, anamkumbuka Raila kwa jinsi alivyompa mapokezi mazuri alipofika nchini katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwai Kibaki akiwa Seneta wa Jimbo la Illinois.

Raila aliandamana na Rais Obama kuelelea Kogelo kwa boma la babu yake alikoishi bibi yake Sarah Obama.

Obama ambaye alikutana na kushirikiana na Odinga hasa alipokuwa Waziri Mkuu wa Kenya amesema pia, ‘maishani mwake, Raila alitoa mfano mkubwa sio tu kwa Wakenya na barani Afrika, bali duniani pia.

Aliongeza: Ninajua wengi watamkosa na kumbuka kwa dhati. Mimi na mke wangu Michelle tunatoa salamu zetu za ramirambi kwa familia yake na raia wa Kenya,’ alimalizia Obama.

Buriani Raila Odinga: Mwili wa Raila Odinga wawasili Kisumu

Jeneza la Raila

Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Amollo Odinga umewasili mjini Kisumu katika eneo la magharibi mwa Kenya na tayari umefikishwa katika uwanja wa michezo wa Jommo Kenyatta Mamboleo.

Raila alianza safari yake ya mwisho duniani kutoka uwanja wa kimataifa wa Jommo Kenyatta jijini Nairobi ambapo alibebwa na ndege ya kijeshi aina ya SPARTAN kutoka kambi ya jeshi la nchi kavu lnalopakana na uwanja wa JKIA.

Shughuli nzima inaongozwa na jeshi la Kenya KDF ambapo maafisa wa kuu wa jeshi wamesimamia usafiri wa mwili huo ambao uliwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kisumu mwendo was aa moja unusu asubuhi.

Ulipokelewa na Meja Jeneali Jospeh Nyaga ambaye ni Afisa msimamizi wa kambi zote za jeshi la nchi kavu katika ukanda wa magharibi mwa Kenya. Luteni Kanali Baraza ambaye ni msimamizi wa maafisa wa jeshi wanaoulinda na kuubeba mwili wa Odinga, alishuka kwenye ndege kwanza na kukikongoza kikosi chacke cha mafias wenye hadhi ya Meja kuandaa jeneza hilo kwa usaidizi wa maafisa wengine wa kijeshi.

Shughuli ya kuondoa mwili kutoka kwa ndege hilyo ya usafiri wa mizigo na wanajeshi kwa shughuli zao za kawaida hapa nchini na vitani, ilikuwa na utaratibu uliofuatwa kwa ufasaha huku wanajeshi wakihakikisha kwamba yote yanakwenda vyema.

Baada ya karibu nusu saaa jeneza lilisukumwa kwa kigari chenye magurudumu mawili makubwa cha kubebea maiti na kupitishwa kwenye angatua hadi upande wa pili ambapo ndege nyingine ya kijeshi aina ya helikopta ya Bell UH -1 ilikuwa inasubiri kuupokea mwili na kuubebba hadi uwanja wa michezo wa Jommo Kenyatta Mamboleo ambao ulikuwa umejaa waombolezaji walioanza kufika pale kuanzia saa kumi za alfajiri.

Ndege hiyo ambayo ilipaa angani kwa muda mfupi tu, kama dakika 8 hivi, wengi wakishangaa kwa nini hatua hiyo ikachukuliwa na serikali.

Huenda idadi kubw aya watu iliyopo kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege wa Kisumu ni mkubwa na vitengo vya usalama havingetaka hali kama iliyoshuhudiwa siku ya Alhamisi kutoka uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta hapa Nairobi kurejelewa.

Wananchi walisimama kando kando ya barabara nje ya uwanja wa Kisumu wakiwa na matumaini ya kuuona mwili ukipita barabarani ila wengi watapata fursa ya kumuaga Raila mwanzo tu shughuli hiyo itakapoanza rasmi hapo mamboleo.

Wakenya watautazama mwili kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na mbili jioni, ambapo Raila Odinga ataanza safari ngumu kabisa ya kuelekea alikozaliwa kule Bondo usiku wa leo na kulazwa katika boma lake la OPODA FARM alikoishi na familia yake.

Odinga atazikwa kando ya baba yake Jaramogi Oginga Odinga – aliyekuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Kenya na aliyefariki 1994. Familia imesema kwamba baada ya ibada ya mazishi itakayoandaliwa Jumapili, ni watu wachache tu watakaoingia katika eneo la makaburini na kushuhudia mwili wake ukishuhswa chini na kuzikwa.

Wananchi watashuhudia shughuli hiyo kwenye runinga kubwa kubwa ambazo zitawekwa katika shule za msingi na upili ambazo ziko karibu na makazi ya KANGO’ KA JARAMOGI ambayo ni boma la mzee Jaramogi na makao ya familia kubwa ya Odinga.

Raila ambaye alikuwa mwanasiasa nchini Kenya aliye na tajriba wa zaidi ya miaka 35, alihudumu kama Waziri Mkuu kati ya 2008 na 2013 ambapo aliwania Urais na kuminyana na Uhuru Kenyatta aliyeshinda uchaguzi huo.

Atakumbukwa kwa mchango wake wa mabadiliko ya kikatiba, uanaharakatiw ake wa kutetea haki za waKenya na juhudi zake za upatanishi ndani nan je ya nchi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply