Wajumbe wa Pakistan na Afghanistan kukutana Doha

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Maafisa wa usalama wa Taliban wakijiandaa kufanya shambulizi la anga mpakaniPicha: Sanaullah Seiam/AFP

Maafisa wa Pakistan watafanya mazungumzo hii leo Jumamosi na wenzao wa Afghanistan huko Qatar, ikiwa ni siku moja baada ya Islamabad kufanya mashambulizi ya angani.

Maafisa wa Pakistan watafanya mazungumzo hii leo Jumamosi na wenzao wa Afghanistan huko Qatar, ikiwa ni siku moja baada ya Islamabad kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya jirani yake. Mashambulizi hayo yamewaua watu 10 na kuvunja makubaliano ya usitishaji mapigano ambayo yalileta utulivu kwa siku mbili katika eneo la mpaka.

Waziri wa ulinzi Khawaja Asif na Mkuu wa ujasusi Asim Malik wanaongoza ujumbe wa Pakistan katika mazungumzo hayo. Serikali ya Afghanistan chini ya Taliban nayo imesema ujumbe wa ngazi ya juu wa nchi hiyo ukiongozwa na waziri wa ulinzi Mohammed Yaqub, unaelekea Doha tayari kwa mazungumzo.

Makubaliano ya masaa 48 ya usitishaji mapigano yalituliza wiki moja ya makabiliano makali ya mpakani ambayo yameua dazeni ya wanajeshi na raia kutoka kila upande.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment