Matamshi ya Kansela Merz yakosolewa kuwa ya kibaguzi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: Niklas Graeber/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wabunge wa upinzani, juu ya matamshi yake ya kufukuzwa kwa wahamiaji yaliyotafsiriwa kuwa ya kibaguzi.

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wabunge wa upinzani, juu ya matamshi yake ya kufukuzwa kwa wahamiaji yaliyotafsiriwa kuwa ya kibaguzi.

Matamshi hayo aliyatoa wakati akijibu swali kuhusu ushawishi wa chama cha siasa kali AfD na juhudi za serikali yake za kurekebisha sera ya uhamiaji. Merz alisema kwamba bado kuna matatizo katika mandhari ya jiji na ndiyo maana waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya shirikisho anatekeleza zoezi la kuwafukuza wahamiaji wengi.

Kauli ya mandhari ya jiji imekosolewa vikali kwa kuonekana kama ya kibaguzi, ikitasfiriwa kuwa maeneo ya mijini ambayo yana wakaazi wa tamaduni mbalimbali kuliko vijijini yanapaswa kulengwa katika kuwafukuza wahamiaji.

Katika barua iliyoandikwa kwa Merz, wanasiasa kadhaa kutoka chama cha upinzani cha Kijani (Greens) wamemtaka aombe radhi hadharani kwa kauli walizoziita za ubaguzi wa rangi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment