UN yasema tani 560 za misaada zinaingia Gaza kwa siku

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Umoja wa Mataifa umesema leo kwamba kwa wastani, tani 560 za chakula zimeingia Gaza kwa siku tangu usitishaji mapigano ulipoanza kutekelezwa.

Misaada ya kiutu katika msafara kivukoni RafahPicha: REUTERS

Umoja wa Mataifa umesema leo kwamba kwa wastani, tani 560 za chakula zimeingia Gaza kwa siku tangu usitishaji mapigano ulipoanza kutekelezwa. Hata hivyo misafara hiyo inatatizika kuufikia mji wa Gaza uliokumbwa na njaa kutokana na barabara kuharibiwa na vita na kuendelea kufungwa kwa njia muhimu kuelekea eneo la kaskazini.

Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher alisema Jumatano kwamba maelfu ya magari ya misaada yatalazimika kuingia kila wiki ili kukabiliana na mzozo unaotokana na utapiamlo, ukosefu wa makazi na kuharibiwa kwa miundombinu.

Shirika la Mpango wa Chakula la WFP limesema kwamba halijaanza usambazaji katika mji wa Gaza, likiashiria kuendelea kufungwa kwa vivuko viwili vya mpakani vya Zikim na Erez, huku Israel ikiwa kaskazini mwa eneo hilo ambako mizozo ya kibinadamu ni mbaya zaidi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment