Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
Takribani asilimia 80 ya watu maskini duniani sawa na karibu watu milioni 900, wanakabiliwa moja kwa moja na hatari za mabadiliko ya Tabia Nchi zinazochangiwa na ongezeko la joto duniani.

Mafuriko ni janga mojawapo la mabadiliko ya tabia nchiPicha: Mohamed Abd El Ghany/REUTERS
Takribani asilimia 80 ya watu maskini duniani sawa na karibu watu milioni 900, wanakabiliwa moja kwa moja na hatari za mabadiliko ya Tabia Nchi zinazochangiwa na ongezeko la joto duniani.
Kulingana na utafiti wa kila mwaka uliochapishwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kwa kushirikiana na mashirika ya Oxford Poverty na Human Development Initiative, watu bilioni 1.1, sawa na asilimia 18 ya watu bilioni 6.3 katika nchi 109 zilizofanyiwa utafiti wanaishi katika umaskini wa kiwango kikubwa.
Utafiti huo uliangazia vifo vya watoto wachanga, upatikanaji wa nyumba, usafi wa mazingira, umeme na elimu. Maeneo mawili yaliyoathirika zaidi na umaskini ni Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara pamoja na Asia Kusini huku pia wakiwa katika hatari kubwa ya kuathiriwa na mabadiliko ya Tabia nchi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.