Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
Rais Donald Trump wa Marekani atakuwa mwenyeji wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy baadae leo ambapo wanatarajiwa kufanya mazungumzo katika Ikulu

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mkutano wa UNGA 2025Picha: Angela Weiss/AFP/Getty Images
Rais Donald Trump wa Marekani atakuwa mwenyeji wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy baadae leo ambapo wanatarajiwa kufanya mazungumzo katika Ikulu. Hata hivyo ishara zinaonesha kwamba Rais Trump hayuko tayari kuiuzia Ukraine makombora ya masafa marefu aina ya Tomahawk, ambayo Ukraine inayahitaji sana.
Mkutano wa Trump na Zelensky unafanyika siku moja baada ya Trump kufanya mazungumzo marefu kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin ambapo walizungumzia mzozo kati ya Urusi na Ukraine na wamekubaliana kukutana hivi karibuni nchini Hungary.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Hungary imesema leo Ijumaa kuwa haitamkamata Rais Putin atakapohudhuria mkutano kati yake na Trump ingawa kiongozi huyo anakabiliwa na waranti wa kukamatwa uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Wakati huo huo pia, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Putin siku ya Ijumaa, kujadili mkutano huo wa kilele utakaofanyika mjini Budapest. Orban ndiye mshirika wa karibu wa Trump na Putin katika Umoja wa Ulaya na mkosoaji mkubwa wa uungaji mkono wa Nchi za Magharibi kwa Kyiv.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.