Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
Makubaliano ya masaa 48 ya usitishaji mapigano kati ya Afghanistan na Pakistan yanamalizika Ijumaa jioni, kufuatia ghasia kubwa baina ya mataifa hayo jirani.

Mzozo wa Afghanistan PakistanPicha: Sanaullah Seiam/AFP
Makubaliano ya masaa 48 ya usitishaji mapigano kati ya Afghanistan na Pakistan yanamalizika Ijumaa jioni, kufuatia ghasia kubwa baina ya mataifa hayo jirani.
Dazeni ya wanajeshi na raia kutoka kila upande wameuawa tangu ghasia zilipozuka karibu wiki moja iliyopita, huku milipuko pia ikisikika karibu na mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
Makubaliano ya usitishaji mapigano yalitangazwa Jumatano huku Pakistan ikiashiria kwamba yatadumu hadi leo jioni. Afghanistan ilisema siku hiyo hiyo kwamba makubaliano hayo yatadumu isipokuwa tu pale Pakistan itakapoyakiuka, bila kudhibitisha kuwa makubaliano hayo yalikuwa na ukomo wa masaa 48.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alisema siku ya Alhamisi kwamba ili suluhu iendelee, mpira unasalia mikononi mwa serikali ya Taliban.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.