Katika maisha haya yenye vita,changamoto na dhiki za kila aina nimejifunza kumwamini Mungu katika hali yoyote ile ninayoipitia
Unaweza kuwa umepoteza kazi,umepoteza marafiki,umepoteza mchumba,umepoteza nafasi mbalimbali ambazo zingekufanikisha
Niko hapa kukwambia mwamini Mungu hata katika mazingira magumu unayoyapitia,Mungu anajua kesho yako imebeba nini kwa ajili yako
Unaweza kudharauliwa,unaweza kuonekana hufai,unaweza kuonekana huna faida,unaweza kuchekwa na watu wako wa karibu katikati ya mambo yote mwamini Mungu
Katika majira na saa usiyodhani,saa ambayo akili zako zimefika mwisho moyo umechoka na mwili wako umechekaa ndipo Mungu unayemwamini atatokea na kukusaidia
Niko hapa kukutia moyo na kukuombea we mwamini Mungu tu atafanya, ninakuombea najua umefika mahali umechoka Mungu unaemwamini ashuke na kukusaidia
Biblia inasema kwenye
Isaya 43:18:19
Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
Sijajua ninani lakini Mungu amenisemesha ya kwamba wako watu ambao kibinadamu wamechoka na akili zao zimefika mwisho
Inawezekana ni kwenye mahusiano umeumizwa mpaka umefika mahali unasema nimefika mwisho sitaki tena,inawezekana ni kwenye ndoa akili zako zimefika mwisho
Moyo wako umejaa maumivu na uchungu uliopelekea hata chakula kukosa radha mdomoni mwako kwasababu ya akili kufika mwisho
Nikiwa katika kuomba na kusali nikasikia sauti ikiniambia sio mwisho, hata kama akili zimefika mwisho Mungu bado hajafika mwisho
Mahali akili za mwanadamu zinapoishia ndipo Mungu anapoanzia inuka tena, Mungu akupe nguvu mpya bado safari inaendalea hapo sio mwisho
Ninakuombea sana Mungu akupe nguvu ya kuinuka tena,ninekuombea Mungu akupe nguvu ya kuendelea tena kesho yako ni nzuri kuliko leo yako sio mwisho songa mbele
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.