Mwili wa Odinga unagwa kitaifa mjini Nairobi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Mwili wa kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga unaagwa kitaifa leo Ijumaa kwa ibada maalamu mjini Nairobi na kuhudhuhuriwa na viongozi wakuu na wawakilishi wa serikali mbalimbali duniani.

Mwili wa Raila Odinga ulipowasili nchini Kenya siku ya Alhamisi ukitokea India.Picha: Andrew Kasuku/AP Photo/picture alliance

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa ibada hiyo itafanyika kwenye uwanja wa michezo wa Nyayo na kuongozwa na Rais William Ruto wa nchi hiyo.

Odinga, mwanasiasa kigogo wa upinzani aliaga dunia siku ya Jumatano akiwa nchini India alikokwenda kwa matibabu.

Mwili wake ulirejeshwa nyumbani jana Alhamisi na maelfu ya watu walipata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye uwanja wa Kasarani nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.

Hata hivyo zoezi hilo lilikumbwa na vurumai iliyosababisha vifo vya watu wasiopungua watatu ya baada ya polisi kufyetua risasiili  kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wakisongamana kuelekea jukwaa la watu mashuhuri.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment