Papa Leo XIV: Kushindwa kuzuia njaa duniani ni dhambi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na:Cantona Joseph|RFA

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV ameikosoa dunia kwa kushindwa kuzuia mamilioni ya watu kufa kwa njaa.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV akifanya ibada huko VaticanPicha: Alberto Pizzoli/AFP

Papa amesema kuruhusu binaadamu wengine wafe kwa njaa ni kushindwa kwa pamoja kuchukua hatua stahiki, ni kupotoka kwa maadili na yote hayo ni dhambi ya kihistoria.

Katika hotuba yake kwenye makao makuu ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP mjini Roma,  Papa Leo XIV  ametoa wito kwa watu kufikiria upya mtindo wao wa maisha pamoja na vipaumbele vyao.

Kauli ya kiongozi huyo wa kidini imetolewa wakati WFP ikitahadharisha takriban watu milioni 319 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kwamba kuna hatari watu milioni 14 wakafariki kwa njaa kufikia mwaka 2030, kutokana na hatua ya mataifa kadhaa kupunguza ufadhili kwa ajili ya misaada ya kibinaadamu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment