Trump kukutana na Zelenskyy baada ya kuzungumza na Putin

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Donald Trump na Vladimir Putin.Picha: ZED

Na:Cantona Joseph|RFA

Rais Donald Trump wa Marekani atakutana na Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine mjini Washington leo siku moja baada ya kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi yaliyojadili hatua za kumaliza vita.

Trump amesema mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Putin “yalikuwa mazuri” na wamekubaliana kufanya mkutano wa kilele mjini Budapest nchini Hungary mnamo wiki zinazokuja.

Atakutana na Rais Zeleskyy katika wakati anatafakari uwezekano wa kuipatia nchi hiyo makombora ya masafa marefu ili kuisaidia kuikabiliana na Urusi.

Inatazamiwa kuwa Zelenskyy atamsihi Trump aidhinishe Ukraine kupatiwa silaha hizo na mifumo zaidi ya ulinzi hasa kutokana na kuendelea kwa mashambulizi ya anga ya Urusi.

Usiku wa kuamkia leo Urusi iliishambulia miundombinu ya umeme ya Ukraine kwa droni na makombora na kusababisha ukosefu wa nishati hiyo muhimu kwenye mikoa kadhaa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment