Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Jamaa za mateka wa Israel wakiandamana mjini Tel AvivPicha: DW
Kundi la kutetea mateka wa Israel limeitaka serikali ya nchi hiyo kuchelewesha hatua zinazofuata za mpango wa amani huko Gaza iwapo Hamas itashindwa kurejesha miili ya mateka waliosalia.
Hata hivyo Israel haijaweka wazi idadi jumla ya miili ya mateka inayotazamia kuipokea. Wito huo umetolewa wakati ambapo serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imetangaza Alhamisi kuwa tarehe ya kufunguliwa kwa kivuko cha Rafah itatangazwa baadaye na kwamba kivuko hicho kitatumiwa pekee kwa harakati za usafiri wa watu.
Kivuko hicho kinachopakana na Misri ni muhimu sana na kilitarajiwa kutumiwa ili kuingiza misaada zaidi ya kibinaadamu huko Gaza . Hayo yakiarifiwa, Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz ametishia kuanzisha tena mapigano iwapo kundi la Hamas litashindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba huo wa amani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.