Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (kushoto) akiwa na rais Donald Trump wa Marekani katika Ikulu ya White House mjini WashingtonPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasafiri kuelekea Marekani ambapo Ijumaa anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump kujadili uwezekano wa kupatiwa silaha zaidi.
Vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa mazungumzo ya Trump na Zelenskyyatajikita katika suala la kuipatia Kiev makombora ya masafa marefu ya Tomahawks na yale ya Patriots.
Hayo yakiarifiwa, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema ataushinikiza Umoja wa Ulaya kutumia mali za Urusi zilizozuiwa ili kuipatia Ukraine mkopo:
” Tunataka kuzitumia vyema mali zilizozuiwa za benki kuu ya Urusi kwa kuipa Ukraine jumla ya euro bilioni 140 kama mkopo wa ziada usiyo na riba.”
Aidha, Ujerumani pia imeahidi kuipatia Ukraine msaada zaidi wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 2 mwaka ujao ili kuiwezesha kuendelea kuikabili Urusi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.