Hakuna mtu ambae hapitii nyakati ngumu, awe masikini awe tajiri kila mtu lazima kuna vipindi vigumu atavipitia katika maisha yake
Kinachotutofautisha ni mitazamo yetu (Attitude) juu ya mambo tunayoyapitia katika maisha yetu
Najua unapopita sio mahali pepesi, najua maumivu uliyonayo moyoni, najua muda uliotumia katika hilo jambo lakini halikukuzalia matunda
Pamoja na mambo yote hayo jifunze sana kubadili mtazamo wako, mitazamo ni kitu ambacho kinaathiri maisha ya watu wengi sana
Watu wengi wanapokuwa katika vipindi vigumu vya kimaisha hujisemesha maneno yanayowasababishia washindwe na wasifanikiwe katika maisha yao
Kuna watu wakiamka tu, huwa wanaanza kujiongelesha ndani yao kuwa
_Hapa nimefika mwisho
_Sijui kama nitavuka tena
hapa
_sijui kama nitafanikiwa tena
_ Hapa lazima nitafeli tu
Hii huwasababishia kuanza siku yao vibaya na kutokuwa na matumaini kabisa ya kufika wanakotaka kufika
Mwalimu wangu alinifundisha hata nipite kipindi kigumu vipi lazima mtazamo wangu uone kushinda na kuanza kukiri ushindi
●Hata kama sioni njia lazima nikiri ushindi mfano hapa lazima nitapita tu
●Hata kama naona giza lazima nikiri ushindi mfano najua mwanga utatokea tu
●Hata kama naona kufeli na kushindwa lazima nikiri ushindi mfano nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu
Je mpendwa wewe huwa unakiri nini unapokuwa kwenye vipindi na nyakati ngumu za kimaisha?
Baada ya kujifunza leo ndani yako unasikia kukiri nini katikati ya mazingira magumu unayoyapitia?
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.