Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius.Picha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images
Na:Cantona Joseph|RFA
Ujerumani imeahidi kuipatia Ukraine msaada zaidi wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 2 mwaka unaokuja ili kuiwezesha kuendelea kuikabili Urusi katika vita vikavyoingia mwaka wa nne.
Tangazo la msaada huo limetolewa na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius mjini Brussels siku ya Jumatano baada ya kukutana na mwenzake wa Ukraine Denys Shmyhal.
Waziri Pistorius amesema wa Ujerumani utatumika kununua silaha za karibu dola milioni 500 kutoka Marekani na kuipatia Ukraine ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga, rada za kijeshi na makombora.
Wawili pia walitia saini mkataba wa kuongeza ushirikiano wa kiulinzi unaojumuisha masuala ya utafiti na maendeleo ya teknolojia.
Ahadi hiyo ya msaada wa kijeshi imetolewa katika wakati serikali mjini Kyiv imesema itahitaji angalau dola bilioni 120 kwa mwaka 2026 zitakazoisadia kuwa na uwezo wa kuendelea kukabiliana na Urusi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.