Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga afariki dunia nchini India akiwa na umri wa miaka 80Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amefariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo nchini India.
Hospitali ya Devamatha katika jimbo la Kerala imethibitisha taarifa za kifo chake hivi leo. Odinga ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 80, aliwahi kugombea urais wa Kenya mara tano katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu.
Mwezi machi, Raila Odinga alikuwa amesaini makubaliano ya kisiasa na rais wa sasa William Ruto ambayo yalikiruhusu chama chake cha upinzani cha ODM kushiriki katika mchakato muhimu wa kupitisha sera huku baadhi ya wanachama wake wakiteuliwa kuwa mawaziri.
Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa na kukitangaza rasmi kifo cha Odinga. Viongozi mbalimbali duniani wameanza kutuma salamu zao za rambirambi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.