Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance
Na:Cantona Joseph|RFA
Iran imesema Jumanne kuwa wito wa rais wa Marekani Donald Trump wa amani na Iran haulingani na vitendo vya Washington, ikiashiria yale mashambulizi ya Marekani katika vinu vyake vya nyuklia mwezi Juni.
Katika taarifa, Iran imesema wito huo unakinzana tabia ya kihalifu inayooneshwa na Marekani kwa watu wa Iran.
Wakati wa hotuba yake katika bunge la Israel, Knesset, hapo jana Rais Trumpalisema anataka makubaliano ya amani na Iran na kwamba kwa makubaliano yoyote kupatikana itategemea Iran yenyewe.
“Na kwa Iran kama mnavyojua, hili halisemwi kutokana na unyonge,hakuna unyonge ila nitasema hivi, tuko tayari nyie mkiwa tayari, na utakuwa uamuzi bora zaidi ambao umewahi kufanywa na Iran, na utafanyika.”
Trump pia alisema itakuwa vyema kama Iran itawacha kuwaunga mkono magaidi, isite kuwatishia majirani zake na iwache kuwafadhili wanamgambo wake na pia itambue haki ya uwepo wa Israel.
Tehran ilimjibu Trump kwa kusema matamshi yake ni ya ovyo na ya kutia aibu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.