Watu 14 wafariki katika mgodi Venezuela

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Mchimbaji migodi huko El CallaoPicha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Na:Cantona Joseph|RFA

Karibu watu 14 wamefariki dunia kufuatia kuporomoka kwa mgodi huko El Callao, Venezuela baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo la kusini mashariki.

Kulingana na shirika la uokoaji vifo hivyo vimetokea katika maeneo matatu tofauti ya mgodi huo wa Cuatro Esquinas de Caratal ulioko karibu kilomita 850 kusini mashariki mwa Mji Mkuu Caracas.

Kulingana na idara ya zima moto ya El Callao, operesheni za kuitafuta miili ya watu hao 14 waliofariki zimeanza na idadi hiyo ya imetokana na ushuhuda wa wachimba migodi wengine.

El Callao ni mji unaotegemea uchimbaji wa dhahabu na idadi kubwa ya wakaazi wake 30,000 wanashiriki uchimbaji migodi moja kwa moja au kwa njia zisizo moja kwa moja.

Venezuela ni nchi iliyo na utajiri wa shaba, almasi na madini mengine ila uchimbaji usio salama ni jambo la kawaida.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment