Jeshi Madagscar latangaza kuchukua madaraka

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Jeshi la Madagascar likipiga doria mitaaniPicha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Na:Cantona Joseph|RFA

Kanali mmoja wa jeshi nchini Madagascar aliyewaongoza wanajeshi kuungana na waandamanaji vijana wanaoipinga serikali, amesema kwamba jeshi limechukua uongozi wa taifa hilo.

Hii ni baada ya Rais Andry Rajoelina kuikimbia nchi hiyo.

Katika tangazo alilolitoa kwenye redio ya taifa, Kanali Randrianirina amesema kuwa jeshi limevunja taasisi zote isipokuwa bunge, ambalo limepiga kura ya kumuondoa madarakani Rajoelina.

Ofisi ya rais imepuuzilia mbali maamuzi ya bunge ikisema  kikao cha bunge kilichopiga kura ya kumuondowa madarakani rais Rajoelina kimekosa  uhalali.

Kura hiyo imeungwa mkono na wabunge 130, hiyo ikiwa zaidi ya thuluthi mbili zinazohitajika katika bunge hilo lenye wabnge 163.

Rajoelina ambaye amekataa kuachia ngazi, alisema amekwenda mahali salama kwasababu ya kutishiwa maisha lakini afisa mmoja wa upinzani, chanzo cha kijeshi na mwanadiplomasia mmoja wa kigeni walisema rais huyo mwenye umri wa miaka 51 aliikimbia nchi Jumapili kwa kutumia ndege ya kijeshi ya Ufaransa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment