UN yataka njia zote za kuingiza misaada Gaza zifunguliwe

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Umoja wa Mataifa na Shirika la Msalaba Mwekundu wametoa wito wa kufunguliwa njia zote za kuingia Gaza, kutoa nafasi ya misaada kuingia katika eneo hilo.

Malori ya kupeleka misaada Ukanda wa GazaPicha: Stringer/REUTERS

Na:Cantona Joseph|RFA

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu  Christian Cardon amefafanuwa dhamira ya  mashirika hayo ya kutaka kuingiza misaada kwa wingi katika ukanda huo wa Gaza.

“Ndio usalama unastahili kuzingatiwa, ila ni pale malori yatakapoingiaUkanda wa Gaza. Ila kabla hapo, kuna hizo njia zakuingia. Kulingana na ninavyojua mimi, si njia zote ziko wazi kwa ajili ya misaada kuingia Gaza na hilo ndilo tatizo kuu kwa sasa. Na hilo ndilo ambalo mashirika ya misaada yamekuwa yakitaka lifanyike, njia zote zifunguliwe kwasababu ya mahitaji makubwa yaliyopo,” alisema Cardon.

Haya yanafanyika wakati ambapo mamlaka  Palestina zinasema sehemu ya kwanza ya miili ya Wapalestina waliouwawa wakati wa vita hivyo vya Gaza, imewasili katika mamlaka hiyo leo baada ya kuachiwa na Israel. Israel bado inaishikilia mamia ya miili ya Wapalestina waliouwawa tangu shambulizi la Oktoba 7 mwaka 2023 wakiwemo wapiganaji walioshirika uvamizi huo na waliopigana baada ya hapo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment