Kongo na M23 wasaini mfumo wa kusimamia usitishwaji mapigano

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda leo wametia saini makubaliano ya kuanzisha mpango wa kufuatilia usitishwaji wa mapigano huko Doha.

Wawakilishi wa serikali ya Kongo na wanamgambo wa M23 huko DohaPicha: Karim Jaafar/AFP

Na:Cantona Joseph|RFA

Haya yamesemwa katika taarifa na wizara ya mambo ya kigeni ya mpatanishi wa pande hizo mbili, Qatar.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Qatar, Marekani na Umoja wa Afrikawatashiriki katika mpango huo kama waangalizi tu.

Doha imesema kuwa mpango huo utasimamia utekelezwaji wa usitishwajiwa kudumu wa mapigano, utachunguza na kuthibitisha ripoti za ukiukwaji na kufanya mawasiliano na pande husika kwa ajili ya kuzuia kurudiwa kwa uhasama.

Makubaliano haya ya leo yanafuatia makubaliano ya usitishwaji mapigano ya awali yaliyotiwa saini na pande zote mbili huko huko Doha mnamo mwezi Julai.

Wanamgambo wa M23 walikuwa wanasisitiza kutafuta makubaliano yao wenyewe ya amani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakidai makubaliano ya DRC na Rwanda yaliyotiwa saini Juni yaliacha masuala ambayo bado yanastahili kuangaziwa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment