Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ni miongoni mwa viongozi 19 watakaoshiriki hafla hiyo katika mji wa Sharm-El Sheikh nchini Misri

Viongozi wanaohudhuria hafla ya kusaini makubaliano ya kusitishwa vita Gaza, nchini MisriPicha: Suzanne Plunkett/REUTERS
Na:Cantona Joseph|RFA
Viongozi wakuu 19 wa nchi na serikali watahudhuria baadae leo mkutano wa hafla ya kusainiwa makubaliano ya amani ya kumaliza vita Gaza, katika mji wa kitalii wa Sharm El Sheikh nchini Misri.
Rais wa Marekani Donald Trump Emmanuel Macron na Waziri mkuu Keir Starmer wa Uingereza pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na rais wa baraza la Ulaya Antonio Costa ni miongoni mwa watakaohudhuria.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ambaye amesema nchi yake itasimamia utekelezaji wa mpango huo wa amani unaoungwa mkono na Marekani, ameelekea Misri kushiriki hafla hiyo ambayo pia itahudhuriwa na rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.