Hamas inawakusanya mateka ‘sasa’, asema Trump, Wapalestina wakirejea kaskazini mwa Gaza

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Kama sehemu ya kwanza ya makubaliano ya usitishaji mapigano ya Gaza yaliyosimamiwa na Rais Trump ina hadi Jumatatu wiki ijayo kuwaachilia mateka wa Israel.

Na:Cantona Joseph|RFA

.

Maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wameanza kutembea kaskazini kando ya barabara ya al-Rashid kuelekea mji wa Gaza ya mpango wa usitishaji vita na kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kuanza kutekelezwa.

Watakachokuwa wakirejelea ni uharibifu uliosababishwa na miaka miwili ya vita.

“Niliiacha familia yangu nyuma na kuanza kutembea kuelekea kaskazini. Maelfu ya watu wanahangaika. Kukodisha gari kunagharimu karibu shekeli 4,000 (£924; $1,227), kiwango ambacho watu wengi hawaweza kumudu.”

Wanaorudi wanasema wanasukumwa na kukata tamaa na wala sio kujiamini kwamba watakuwa salama. Baadhi yao tayari wameambiwa kwamba nyumba zao hazipo tena.

Kulingana na uchanganuzi wa picha za satelaiti uliotolewa mapema mwezi huu kutoka kwa watafiti katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Oregon, majengo 198,883 katika Ukanda wa Gaza yanakisiwa kuharibiwa tangu kuanza kwa vita.

Uharibifu wa majengo unaweza kuonekana katika eneo lote, huku Jiji la Gaza likiwa mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi.

Watafiti wanakadiria kuwa 74% ya majengo katika eneo hilo yaharibiwa tangu 7 Oktoba 2023.

Marekani kuwapeleka wanajeshi 200 Israel kufuatilia usitishaji mapigano Gaza

.

Takriban wanajeshi 200 wa Marekani ambao tayari wako Mashariki ya Kati watapelekwa Israel ili kusaidia kufuatilia usitishaji mapigano Gaza, kwa mujibu wa maafisa wa Marekani.

Jeshi la Marekani litaanzisha kikosi kazi cha kimataifa nchini Israel, kinachojulikana kama kituo cha uratibu wa kijeshi wa kiraia, ambacho huenda kikajumuisha wanajeshi kutoka Misri, Qatar, Uturuki na UAE, walisema.

Afisa mmoja mkuu alisema hakuna vikosi vya Marekani vitaingia Gaza, akiongeza kuwa jukumu la Marekani lilikuwa kuunda Kituo cha Udhibiti wa Pamoja ambacho “kitaunganisha” kikosi cha kimataifa kinachoingia.

Kikosi kazi hicho kitaongozwa na Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) yenye makao yake makuu katika eneo hilo, na inanuiwa kusimamia makubaliano ya kusitisha mapigano na pia kusaidia kuratibu misaada ya kibinadamu.

Waziri wa mambo ya ndani wa Cameroon awaonya wagombea kutojitangaza washindi wa uchaguzi

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cameroon Paul Atanga Nji
Maelezo ya picha,Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cameroon Paul Atanga Nji

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cameroon Paul Atanga Nji amewaonya wagombea wanaoshiriki uchaguzi wa rais Jumapili dhidi ya kudai ushindi kabla ya matokeo rasmi kutangazwa na baraza la katiba.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa kabla ya upigaji kura, Nji alidai kuwa amepokea taarifa zikionyesha kwamba kuna mgombea anapanga kujitangaza mshindi japo hakumtaja mgombea huyo.

Nji alilitaja wazo hilo kuwa “limepitwa na wakati” akitishia kumchukulia hatua yeyote atakayefanya hivyo.

“Wale ambao watajaribu kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais au ushindi wowote wa kujitangaza wenyewe kwa kukiuka sheria za jamhuri watakuwa wamevuka mstari mwekundu,” alionya.

“Wagombea lazima watumie njia za kisheria kutetea haki zao,” alisema.

Hapo awali, waziri huyo alidai kuwa baadhi ya wagombea wa upinzani walikuwa wakipanga njama ya kuvuruga mchakato wa uchaguzi kupitia maandamano na kughushi matokeo.

Mnamo 2018, Paul Biya alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa 2018.

Lakini kiongozi wa upinzani Maurice Kamto alidai kura hizo ziliibiwa na kumuunga mkono mgombea aliye madarakani, akidai ndiye mshindi halali.

Melania Trump asema ameanzisha mchakato wa ‘mawasiliano’ na Putin kuhusu watoto wa Ukraine

Melania Trump
Maelezo ya picha,Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump

Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump anasema Rais wa Urusi Vladimir Putin amejibu barua aliyomuandikia kuelezea wasiwasi wake kuhusu watoto wahanga wa vita vya Urusi na Ukraine.

Alitoa tangazo hilo siku ya Ijumaa, akisema kwamba baada ya ” mawasiliano ya wazi” na Putin, watoto wa Ukraine waliokuwa wamepoeleana na wazazi wao wakati wa vita wameunganishwa tena na familia zao.

“Barua ya amani” ya Mke wa Rais iliwasilishwa kwa mkono kwa Putin wakati wa ziara yake huko Alaska mnamo mwezi Agosti.

Rais Donald Trump aliweka sehemu za barua hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Katika barua hiyo, Melania Trump anamsihi Putin kuwalinda watoto, akiongeza kwamba kufanya hivyo “kutafanya hivyo sio kwa maslahi ya Urusi pekee” bali ni “kuonyesha moyo wa ubinadamu”.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment