Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Yvette Cooper ni mwenyeji wa mkutano wa washirika wa Ulaya.Picha: Yuki Iwamura/AP Photo/picture alliance
Na:Cantona Joseph|RFA
Uingereza ni mwenyeji wa mkutano unaohusu usalama na uhalifu wa wahamiaji katika eneo la Balkan Magharibi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Yvette Cooper atakuwa mwenyeji wa mkutano wa washirika wa Ulaya utakaozungumzia juu ya uhalifu wa wahamiaji na usalama katika nchi za eneo la magharibi la Balkan huku serikali ikitafuta njia za kukabiliana na ongezeko la wahamiaji katika vivuko vidogo vya mashua.
Uingereza itaahidi ufadhili wa kuimarishwa kwa usalama na sheria mpakani, mafunzo ya utekelezaji wa sheria nchini Kosovo pamoja na msaada wa kuimarisha ulinzi wa mtandao dhidi ya tishio la kuingiliwa na Urusi katika eneo hilo.
Cooper atakutana Alhamisi na washirika kutoka nchi zikiwemo Albania, Serbia, Macedonia Kaskazini, na Bosnia Herzegovina pamoja na washirika wa Ulaya kama vile Ufaransa, Ujerumani na Italia.
Katika mkutano huo utakaofanyika katika kasri la Hillsborough – mahali yaposainiwa Makubaliano ya Amani ya Ijumaa Kuu – Cooper atatangaza ufadhili wa pauni milioni 4 ($ 5.3 milioni) kusaidia kupambana na vitisho vya Urusi vinavyolenga “kuliyumbisha eneo hilo na “kuchochea mivutano ya kikabila.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.