Usighairishe tena leo!

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Miaka kadhaa huko nyuma, siku moja nikiwa naongea na Mentor wangu, aliniuliza kwa nini hivi vitu ulisema utafanya haujaanza kufanya?

Nikamjibu kwa kujiamini…

“Bado nina muda nitafanya next year”.

Akanigeukia akaniangalia kwa jicho la UKALI, kisha akaniuliza…

“What if tommorow is not yours?”

(Itakuwaje kesho isipokuwepo?).

Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa na ikanipa tafakari ya ndani sana.

Niligundua kuwa, Ingawa kuna mambo sijaanza kuyafanya kwa sababu ya kukosa rasilimali…

…ila yako mengi ambayo siyafanyi kwa sababu NIMERELAX kwa kufikiria kuwa nina MUDA MWINGI sana.

Hivi umeshawahi kujiuliza, Kama ungekuwa unajua kuwa…

…una muda mchache wa kutekeleza ndoto zako, ungeendelea kughairisha?

Watu wengi umri wao unapokuwa umeenda sana, huwa wanajutia zaidi…

…mambo ambayo HAWAYAKUYAFANYA kuliko yale ambayo WAMEYAFANYA.

Leo, tafakari kuhusu zile NDOTO unazoendelea kusogeza mbele…

Kuhusu yale MAAMUZI unayosubiria muda sahihi…

Kuhusu zile HATUA ambazo UNASITA kuzichukua kila siku.

What if tommorow is not yours?

Vipi kama hiyo kesho unayoisema hautakuwepo.

Fanya maamuzi kumaximise leo yako ili hata ikitokea kesho sio ya kwako…

…utakuwa tayari umefanya yaliyo ndani ya uwezo wako.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment