Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA
(Wateja Wanaona Hivyo Na Unahitaji Kubadilika.)
Kuna vitu vidogo unavyofanya kila siku ambavyo vinafukuza wateja kimya kimya.
Wateja hawasemi moja kwa moja wanatabasamu, wanaondoka… halafu hawarudi tena
Kama unafanya haya mambo, tafadhali anza kubadilika leo.
…
1. KUKOSA MZIGO MARA KWA MARA
Wateja wakija mara tatu mfululizo na hukuti na bidhaa wanahamia kwa mwingine.
SULUHISHO: Panga stoo yako vizuri na fuatilia bidhaa zinazouzwa haraka.
…
2. KUKOSA CHENJI KILA SIKU
Wateja wanapochanganyikiwa kila mara “subiri nikaangalie chenji, wanachoka.
SULUHISHO:Tengeneza mfuko maalum wa chenji kila asubuhi.
…
3. KUFIKA KAZINI MUDA UNAOTAKA.
Wateja wanapokuja hukuti kazini wanahisi huna nidhamu.
SULUHISHO: Weka ratiba thabiti na iheshimu kama mtu wa ofisini.
…
4. HUDUMA ISIYO NA FURAHA
Mteja anapokuliza bei na unamjibu kwa hasira au kutojali anakutafsiri vibaya.
SULUHISHO: Tabasamu, ongea vizuri, na toa huduma bora kila wakati.
5. KUTOJIBU SIMU AU MESEJI ZA WATEJA
Kama mteja anakupigia au kutuma DM na hupatikani anatafuta mwingine papo hapo.
SULUHISHO:Weka muda maalum wa kujibu meseji na simu. Kuwa active.
…
6. KUKOSA MAWASILIANO BAADA YA MAUZO
Baada ya kuuza, unanyamaza, haufuatilii wala kuuliza kama bidhaa ilimfaa.
SULUHISHO:Fanya follow-up fupi kwa shukrani au mrejesho.
…
7. BEI KUBADILIKA BILA MPANGILIO
Leo bei ni hii, kesho ni nyingine bila sababu au maelezo. Unafukuza wateja wako..
SULUHISHO: Weka bei thabiti na tangaza mapema kama kuna mabadiliko.
…
8. MAHALI PASIPO SAFI AU MPANGILIO MBAYA
Hata bidhaa nzuri zikipangwa ovyo, wateja hawana hamasa ya kununua.
SULUHISHO: Safisha eneo la biashara kila siku; mpangilio mzuri huvutia macho.
…
9. KUWAFANYA WATEJA WASUBIRI SANA
Huduma zinachelewa bila sababu, huku wateja wengine wanaona unacheka tu.
SULUHISHO: Jifunze kupanga muda, au tafuta msaidizi wakati wa msongamano.
…
10. KUTOKUWA NA MAARIFA KUHUSU BIDHAA ZAKO.
Wateja wanakuuliza swali rahisi, hujui kujibu. Wanahisi huna uelewa.
SULUHISHO: Jifunze kila kitu kuhusu bidhaa zako uwe mtaalamu wa kile unachouza.
Wateja hawakimbii bei wanakimbia uzoefu mbaya.Ukirekebisha haya mambo 10 madogo, biashara yako itaonekana ya kitaalamu, yenye nidhamu, na inayojali.
Wateja watarudi, na wataleta wengine.
Ni jambo gani ambalo bado unahitaji usimamizi kati ya haya?
Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.