USALAMA WA NDOTO.

Baada ya utangulizi wa sehemu ya kwanza leo napenda niingie kwenye maandiko machache yanasamaje kuhusu ndoto?

Ni kweli kwamba ndoto imekuwa ni njia mojawapo ambayo watu wakuu wa Mungu waliitumia kuweza kuelewa sauti ya Mungu, na jambo jema ni kwamba walifanya vizuri kwa kuwa na usahihi wa ndoto na tafsiri zake kiasi zilileta matokeo mazuri. Rejea Daniel na Yusufu ambao sio tu kwamba waliota bali walitafsiri ndoto kwa KURUDI KWA BWANA NA KUULIZA MAANA YAKE NA MUNGU ALIWAPA unaweza soma Mwanzo 37:5, 41:1…. pia Daniel 7:1-28.

Kama ndoto ilitumika kwa wakati ule hata sasa inaweza kutumika, lakini njia ipi au ni vipi tutafanya ili tufanikiwe ndoto zetu ziwe na maana iliyokusudiwa na namna gani tutapata tafsiri sahihi na sio kubabaisha na mwisho kuchanganyikiwa?

Kwanza kabla hatujajibu swali hilo naomba nikupe andiko hili

Mith 14:4

Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi.

Mwandishi wa mithali anajaribu kutuonya kuhusu zizi na ng’ombe ILI TUWEZE KUFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KUCHAGUA AMA ZIZI KUWA SAFI AMA NGUVU ZA NG’OMBE, ILA ANGALIZO NI KWAMBA NG’OMBE ANACHAFUA ZIZI. Rejea sababu zangu kwenye sehemu ya kwanza, NILIAMUA KUACHANA NA MAISHA YA NDOTO ILI NILIACHE ZIZI LANGU SAFI. Niliona ni heri nikose faida za ng’ombe maana alinichafulia zizi. Hii haina maana kuwa hawapo watu wenye misuli ambao wanaweza kufaidika na ng’ombe na wakati huohuo wakawa na bidii ya kusafisha zizi ili wapate vyote. KWA MANTIKI HIYO MAFUNDISHO KUHUSU NDOTO NI MOJA YA NJIA BORA YA KUSAFISHA ZIZI ILI TUMFAIDI NGOMBE NDANI YA ZIZI SAFI.

Faida na hasara za maamuzi haya.
Faida za zizi safi lisilo na ng’ombe.
1. Litabaki na usafi wake maana yule anayetakiwa kukaa ndani yake amekataliwa.

2. Litabaki na harufu nzuri.

3. Litakuwa na utulivu
4. Halitalegea maana halina matumizi tarajiwa.
5. Ukarabati wake utakuwa nafuu.

Hasara.
1.litapoteza maana ya kimatumizi, kwa sababu halifanyi kazi tarajiwa.

2. Litakosa nguvu ya ng’ombe ambayo lilijengwa kumuhufadhi.

3. Litakuwa tupu
4. Linaweza badili matumizi toka ya asili na kuwa na matumizi mapya.

Faida za Ng’ombe
1. Chakula, kama maziwa nk vitakauwepo.

2. Uwepo wake utaongeza tija kwa mfugaji. Maana aweza Lima nk

3. Ataongeza shughuli na pilikapilika nyumbani.
4. Atakuwa chanzo cha pato la kiuchumi.

Hasara
1. Atachafua zizi
2. Harufu ya eneo NA zizi haitakuwa kama kawaida , atachafua hewa

3. Aweza kuwa chanzo cha magonjwa
4. Ataongeza kelele nk
5.Ataongeza gharama ya matunzo

UKIZIANGALIA FAIDA NA HASARA (nyingine utaongezea kulingana na unavyojua) UTAGUNDUA NI BORA TUMTUMIE NG’OMBE LAKINI TUKUBALI NA TUJIANDAE KUWA SMART NA KUWA NA BIDII NA UVUMILIVU KUFANYA KAZI ILI TUWEZE KUPATA VYOTE ZIZI SAFI NA FAIDA ZA NG’OMBE.

NAMNA GANI TUTAFANIKISHA HILI?

1. NI LAZIMA TUJUE CHANZO CHA NDOTO (NG’OMBE WETU) ILI KULINDA ZIZI (KANISA, MAHUSIANO, NDOA, MOYO, JAMII, UONGOZI, KAZI NK)

Kuna namna tatu ambazo ndio chanzo cha kila ndoto, kama hakitakuwa hiki basi ni kile. Chanzo cha ndoto kinaweza kuwu, MUNGU, SHETANI AU MTU MWENYEWE kama ifuatavyo.

a) Mungu
Ukisoma maandiko utagundua Mungu amekuwa chanzo cha ndoto. Mara nyingi ameongea kupitia ndoto na watumishi wengi mfano, Yusufu, Mwanz 37:4,9. 41: 25
Daniel 7:1-28
Abimeleki mwanz 20:3
Wafungwa Gerezani mwanz 40:8
Farao mwanz 41:2
Yusufu wa Maria math 2:13. 1:20-23
Hes 12:6 kwa nabii.
Ayub 33:14-18
Huu ni ushahidi baadhi tu wa Biblia kuthibitisha Mungu huongea kupitia ndoto.

b) Shetani
Kuna ushahidi mwingi tu wa maandiko kuthibitisha shetani aweza kuwa chanzo cha ndoto.
Zek 10:2 ndoto za uongo.
1yoh 4:1, pimeni roho kama zimetoka kwa Mungu, ina maana kinyume chake ni kweli.
2kor 11:14 Hujigeuza malaika wa nuru.
Uf 20:10 Nabii wa uongo
Zek 3:1 shetani alionekana kwenye ndoto akimnyemelea Kuhani Mkuu.
Hiyo ni baadhi ya mistari michache inayohitaji umakini wa kuisoma na kukuyhibitishia kuwa shetani aweza kabisa kutumia ndoto kumsemesha mtu.

c) MTU mwenyewe
Mhu 5:3 Ndoto huja kwa shughuli nyingi.
Isa 29:8 Nia ya mtu mbaya inavyoweza mpa ndoto
Iangalie mistari hii kwa makini utagundua kutokana na mahangaiko na shughuli za binadamu Mara nyingi sana ndoto zake zitakuwa nyingi.

Na hiki ni chanzo kikubwa zaidi kinachoruhusu ndoto za kila aina, iwe toka kwa Mungu, shetani au Mtu mwenyewe.Atahitajika huyu kuzipa nafasi na kuzipokea kisha kuzitendea KAZI ama kuziacha MAANA AMEPEWA UHURU WA KUCHAGUA NA KUAMUA MAMBO YAKE.

Kama hivyo ndivyo basi KUNA HAJA TENA KUBWA YA MTU HUYU KUANDALIWA TENA KWA MAFUNDISHO JINSI YA KUKABILIANA NA NDOTO/CHANZO. ILI AWE SALAMA YEYE, NA WENGINE WATAKAOHUSISHWA NA NDOTO ZAKE.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment