Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moshi unafuka baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kulenga maeneo ya makazi katika Ukanda wa Gaza, kama inavyoonekana kutoka Israel karibu na mpaka, Oktoba 07, 2025.
Na:Cantona Joseph|RFA
Mjumbe mkuu wa Hamas, Khalil El-Hayya, amesema kundi hilo linataka dhamana kutoka kwa Rais wa Marekani Trump na nchi zinazodhamini kuwa vita vitamalizika kabisa.
Katika mazungumzo ya Misri yasiyo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel, Mjumbe mkuu wa Hamas, Khalil El-Hayya, amesema kundi hilo ‘linataka dhamana kutoka kwa Rais wa Marekani Trumpna nchi zinazodhamini kuwa vita vitamalizika kabisa mara moja na daima baada ya makubaliano kuridhiwa.
Katika mahojiano yake na kituo cha Al Qahera amesema hawana imani na Israel hata kidogo. Akisema Israel haijawahi kutimiza ahadi zake katika suala la uvamizi katika historia. Ameongeza kwa kusema wameshuhudia hilo mara mbili katika vita vita hivi vinavyoendelea. Kwa hiyo, wanahitaji dhamana ya kweli.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.