USALAMA WA NDOTO

Namshukuru sana Mungu kwa ajili ya watumishi wa Mungu wengi waliopata neema ya kufundisha somo la ndoto, kwa maoni yangu naona ni jambo jema sana kuwafundisha watu mambo haya MAANA NI MOJA YA ENEO LENYE CHANGAMOTO SANA KWA WANA WA MUNGU.

Nimeguswa pia kukumbusha jambo kwa watu wa Mungu kuhusu ndoto, NA NDIO MAANA KICHWA CHA HAPO JUU NIMEKIPA, “USALAMA WA NDOTO”

Kwa nini USALAMA WA NDOTO?
Kabla sijaendelea naomba nitoe uzoefu wangu binafsi, Mimi sio shabiki kabisa au muumini wa maisha ya ndoto, kwa sababu zimewahi kunichanganya binafsi, na nimewahi ona watu wengi wakichanganyikiwa na nimeona kanisa likiyumba na kuvurugika kisa ni ndoto. NDIO MAANA NIMESHUKURU MUNGU KUONA SASA ANASAIDIA WATU WAKE KUPITIA WAALIMU KUHUSU ENEO HILI MUHIMU LA NDOTO.

Nini kilitokea?
Kisa cha kwanza.
Binafsi nimewahi kujaribu kuishi na kuendesha mambo yangu kwa ndoto ila kilichonikuta kilinifanya nibadilishe mtazamo na kuondoka kabisa, MAANA MATOKEO YAKE HAYAKUWA MAZURI KWANGU, NADHANI LABDA KWA SABABU SIKUWA NA FUNDISHO LA MSINGI KUHUSU NDOTO NA MWAMINI.

Ilikuwa hivi, miaka ya nyuma nikiwa mdogo mdogo, wokovu ndio umeshika kasi, nilitamani sana Mungu awe anasema na Mimi, na niliamini kabisa moja ya njia muhimu ya Mungu kusema nami ilikuwa ndoto, na ukweli nilipenda Mungu aseme nami kwa njia hiyo, na kwa sababu hiyo nilianza kujiandaa, kusikia na kupokea sauti ya Mungu.

Na sikuishia hapo nilifika hatua ya kuunda timu ya maombi niliyoipa jina TIMU YA MAOMBI YA KINABII, na msingi wetu ulikuwa ndoto, kwa hiyo ile team ya watu watano kila ilipokutanika masimulizi ya ndoto na tafsiri ndio yalikuwa msingi wa kujua nini Mungu anasema.

Siku moja nikaanza kuona tatizo baada ya kuanza kujihisi Mimi kila nachokiota ndio sahihi, hivyo nikaanza kutokubali ndoto ya mwingine maana nilianza kuhisi za kwao zina walakini ila zangu ni sahihi. KITU AMBACHO HATA KAMA KINGEKUWA CHA KWELI BADO UKWELI WAKE HAUKUWA NA MSINGI WA KIMUNGU, MAANA TAYARI ROHO YA KIBURI ILISHAANZA KUINUKA NDANI YANGU.

Tatizo la pili, siku ingine aliinuka mmojawapo wa wanateam baada ya kuona ndoto yake haisikilizwi akaja na style mpya ya “BWANA ASEMA, NYAMAZENI MNISIKILIZE” na tuliponyamaza akasema ndani ya team yetu kuna mchawi. Na bahati mbaya sana kulikuwa na mwenzetu ambaye background yake ilishakuwa na tuhuma, bibi zake walishawahi kutuhumiwa uchawi kwenye mtaa wake, na huyu ndugu akanyoosha mkono kwa ukali na kusema fulani ni mchawi mwondoeni anaharibu uwepo wa Mungu. YULE MWENZETU TULIMUUMIZA SANA MAANA TULIANZA MAOMBI YA KUFUKUZA MCHAWI TENA KWA KUMSHIKA HADI KICHWANI, BAADAYE TUKAGUNDUA KUNA JAMBO TUNALIFANYA HALIKO SAWA.

Tulitumia hekima na kukaa na yule ndugu lakini tukagundua aliota, hivyo njia pekee ya kutushinikiza tuamini ni kwa kusema Bwana Asema. KUMBE ILIKUWA NDOTO ALIYOOTA.
Sikumlaumu ila nilijilaumu kwa sababu naliona kabisa hatukuwa na fundisho sahihi kuhusu ndoto, na hatukujua namna gani tunaweza KUJUA SAUTI IPI NI YA MUNGU NA IPI SIO, KWENYE NDOTO ZETU.

Mkasa wa pili.
Huu nilishuhudia Kanisa la Bwana likimeguka vipande viwili. Ambapo aliinuka mwotaji ndoto na akasema alichukuliwa akapelekwa kuzimu kwa ndoto, na akaonyeshwa viwanda vya mafuta, nguo, perfume na urembo mwingi, iliwemo vipodozi ambavyo vimetengenezwa kwa kuharibiwa mimba za watoto wachanga, na SHETANI MWENYEWE AKAMWAMBIA WOTE WANAOTUMIA HIVYO VITU HAWATAENDA MBINGUNI.

Nakumbuka nilikuwa moja ya vijana viongozi wadogo na nisio na ushawishi, na bahati nzuri kipindi hiki tayari nilishashtukia biashara ya ndoto, UKWELI NILITEGEMEA VIONGOZI WAKUBWA WANGEONA WALAKINI ULIOKUWEMO KWENYE NDOTO NZIMA, MAANA PAMOJA NA KUWA MSIMAMO WETU ULIKUWA HATUKUBALIANI NA HIVYO VITU HATA KABLA HAJAOTA, ILA SIKUWA NA AMANI KUONA ALIYEMWAMBIA KUHUSU YALE MAPAMBO NI SHETANI TENA KUZIMU.

Bahati mbaya hakuna aliyesikiliza kwa sababu ile ndoto ilikuwa na sadaka ya ukombozi ndani yake ambayo wengi walitoa kujikomboa na vipodozi walivyokwisha kuwa wamevitumia. SIKUWA NAA SHIDA NA MATOKEO ILA NILITATIZWA NA CHANZO KILICHOLETA MATOKEO YALE.

Hii ilinifanya niendelee kuona nahitaji kumtafuta Mungu zaidi na kujengwa KWENYE msingi imara badala ya kuishi kwa ndoto AMBAZO MIMI BINAFSI NILIZIONA HAZINA MATOKEO CHANYA KWANGU NA KWA MWILI WA KRISTO( KANISA). Hasa kama kanisa halitaamua kupima ndoto/unabii kabla hawajafanya maamuzi ya kuufuata ama kuukataa.

Kisa cha tatu
Nimewahi shuhudia chumba, ndoa na hata mahusiano mazuri na yenye afya, yakivunjika ama kuingia dosari kubwa, tena mengine dakika ya mwisho, KISA MMOJA YA WANAMAHUSIANO AU KAOTA AMA KAAMBIWA NA MWOTAJI, kuwa uchumba, ndoa, au mahusiano na hata kazi SIO MPANGO WA MUNGU.

Na hili likapelekea kuvunjika, ama kuachana na baada ya Muda hali yao ya pili kuwa mbaya zaidi ya ile ya kwanza, NA WANAPOGUNDUA NDOTO HAIKUWA SAHIHI NA HAIKUTOKA KWA MUNGU, WANAKUWA WAMECHELEWA SANA NA GHARAMA YA KUWAFANYA WARUDI KWENYE MSITARI IMEKUWA NGUMU KUPITA KAWAIDA.

Kwa sababu za visa vyote hivyo, moyo wangu umekuwa ukitaabika sana, mpaka kufikia hatua ya kusema SITAKUWA SHABIKI WA NDOTO, NA NINAPOONA HATA MTU ANAKUJA KUNIOMBA NIMSAIDIE MAANA YA NDOTO YAKE, UKWELI HUWA NAKWEPA SANA. MAANA NILISHAKUTWA NA MASHAKA MAKUBWA NA SITAKI KUHUSIKA TENA NA MAMBO HAYA MPAKA PALE NITAKAPOKUWA NIMEBORESHA SANA MAMBO YA ROHONI KUWEZA KUMUDU HALI ZOTE.

NATAMANI NIINGIE KWENYE MAANDIKO BAADA YA UTANGULIZI HUU, ILI NIWE SEHEMU YA WATUMISHI WA MUNGU, WAALIMU WALIOPATA NEEMA KUFUNDISHA SOMO HILI, NAMI NIWEZE KUFUNDISHA KWA SEHEMU KILE MUNGU ALINISAIDIA. ILI MWILI WA KRISTO UKIELEWA BASI TUPATE USALAMA WA NDOTO, TUWEZE KUMSIKIA MUNGU, NA NDOTO ZISIWE TENA CHANZO CHA MISIBA ISIYOISHA..


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment