WHO yaonya juu ya sigara za kieletroniki kwa watoto

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

vc

Na:Cantona Joseph|RFA

Shirika la afya Duniani WHO limeonya kuwa sigara za kieletroniki zinachochea kwa kiasi kikubwa wimbi la uraibu huku ikiripotiwa mamilioni ya watoto wametumbukia kwenye uraibu wa kuvuta sigara hizo za kieletronii.

WHO inasema nchi zinazokusanya data zinaonesha kuwa watoto wako katika hatari mara tisa ya kutumia sigara za kieletroniki kuliko watu wazima.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema wauzaji sigara hizo wananadi kuwa hazina madhara sana kama sigara za kawaida, na wanawalenga sana vijana na kuwafanya kutumbukia kwenye uraibu wa kutumia sigara.

Kulingana na makadirio ya kwanza yaliyofanywa na WHO kuhusu matumizi ya sigara za kieletroniki, zaidi ya watu milioni 100 wanavuta kati ya hao, milioni 86 ni watu wazima hasa wanaotokea mataifa matajiri lakini pia takwimu hizo zinaonesha watoto milioni 15 wa kati ya umri wa miaka 13 hadi 15 wanatumia sigara hizo.

Kwa jumla idadi ya wanaovuta sigara imeshuka duniani kutoka bilioni 1.3 ilivyokuwa mwaka 2000 hadi bilioni 1.2 mwaka 2024. Hata hivyo kati ya watu wazima watano ulimwenguni, mmoja ni mraibu wa sigara.

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema mamilioni ya watu wanaacha au hawaoni haja ya kuanza kuvuta sigara, jambo ambalo limechochewa na juhudi za kudhibiti matumizi ya bidhaa hiyo. Inaripotiwa kuwa wanawake wengi wanaacha kuvuta sigara ikilinganishwa na wanaume.

Umoja wa Mataifa unaonya matumzi ya sigara yanaua zaidi ya watu milioni saba kila mwaka huku wanaoishi katika mazingira ya wavutaji sigara, takribani milioni moja pia hufa kila mwaka.

Naibu mkurugenzi mkuu wa WHO Jeremy Farrar amesema uvutaji wa sigara huharibu kila kiungo cha mwili na kusababisha magonjwa hatari na vifo vya mapema.

Farrar ameongeza kusema takriban watoto milioni 40 wanatumia sigara, huku katika baadhi ya mataifa, watoto wa chini ya umri wa miaka kumi wameanza kutumia sigara na imechochewa kwa kiasi kikubwa na matangazo ya kibiashara mitandaoni ambayo mara nyingi wanatumia watu wenye ushawishi kwa njia ambayo haitangazi moja kwa moja uvutaji wa sigara lakini wanajifanya kujadili masuala mengine huku wakivuta sigara za kieletroniki.

Jaji arushiwa kiatu kwa matamshi yake kuhusu Mungu wa Kihindu

we
Maelezo ya picha,Jaji Mkuu wa India BR Gavai

Wakili wa India amemrushia kiatu Jaji Mkuu wa nchi hiyo BR Gavai baada ya kukasirishwa na matamshi ya jaji huyo kuhusu mungu wa Kihindu.

Rakesh Kishore alirusha kiatu wakati wa kesi ya Jumatatu katika mahakama ya jiji la Delhi.

Mawakili watatu waliokuwepo katika chumba cha mahakama waliithibitishia BBC kwamba kiatu kilirushiwa kwa hakimu, huku mmoja akisema “kimemparaza hakimu mkuu na hakimu mwingine na kuanguka nyuma yao”.

Bw Kishore alisikika akisema “India haitavumilia matusi kwa Sanatan Dharma [Uhindu]”, alipokuwa akitolewa nje ya chumba cha mahakama na maafisa wa usalama. Baadaye alisimamishwa kufanya kazi.

Jaji Mkuu Gavai alibaki mtulivu wakati wote, Anas Tanwir, wakili mwingine aliyekuwa katika chumba cha mahakama, aliambia BBC.

Jaji mkuu hajatoa maoni hadharani kuhusu suala hilo.

Serikali ya India imesema hakuna mashtaka ambayo yangefunguliwa dhidi ya Kishore.

Akiongea na kituo cha habari cha India cha The Print, Bw Kishore alisema kisa hicho kilihusiana ombi lililokataliwa na jopo la mahakama kuhusu sanamu la mungu wa Kihindu Vishnu.

Akitupilia mbali ombi la kujenga upya sanamu ya futi saba ya Vishnu kwenye hekalu katika jimbo la Madhya Pradesh mwezi uliopita, jaji mkuu alisema: “Nenda kamuombe mungu mwenyewe afanye jambo.”

Maoni hayo yalizua utata, huku wengine wakimshutumu kwa kukejeli imani ya Kihindu. Jaji Gavai baadaye alijibu ukosoaji huo, akisema anaheshimu “dini zote,” Press Trust of India iliripoti.

“Hakukataa tu kukubali maombi, bali alimdhihaki

Vishnu,” Kishore aliambia gazeti la The Print.

Kumrushia mtu kiatu hadharani kunaonekana kuwa ni kitendo cha kukosa heshima na udhalilishaji nchini India na nchi nyingine nyingi.

Mapema mwaka huu, Rais wa Kenya William Ruto alirushiwa kiatu wakati wa maandamano.

Mnamo mwaka 2008, mwandishi wa habari wa Iraki alimrushia kiatu Rais wa wakati huo wa Marekani George W Bush akipinga uvamizi wa Marekani nchini Iraq.

Wadukuzi wa Korea Kaskazini waiba kiasi kikubwa cha pesa – watafiti

gb

Wadukuzi wanaohusishwa na utawala wa Korea Kaskazini wameiba zaidi ya dola za kimarekani bilioni 2 (£1.49bn) kulingana na watafiti wanaosema mwaka 2025 ni mwaka ambao wizi hao wamevunja rekodi.

Wizi huo sasa unachangia karibu 13% ya pato la taifa la nchi hiyo (GDP), kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

Mashirika ya usalama ya nchi za Magharibi yanasema fedha hizi zinatumika kufadhili mipango ya kutengeneza silaha za nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini.

Katika miaka ya hivi karibuni, wadukuzi kutoka katika timu za udukuzi kama vile Lazarus Group wamekuwa wakilenga kuiba sarafu za mtandaoni kwa wingi.

Mashambulizi mabaya zaidi kati ya haya yalitokea Februari mwaka huu wakati wadukuzi walipoiba dola bilioni 1.4 kutoka kampuni ya pesa za kidigitali ya ByBit .

Lakini utafiti mpya kutoka wachunguzi wa kampuni ya Elliptic unaonya wahalifu wa mtandao wanazidi kuwalenga watu ambao wana kiasi kikubwa cha pesa za mtandaoni.

Ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza ulitafutwa ili kutoa maoni yake lakini haukujibu. Hapo awali serikali hiyo ilikanusha kuhusika na udukuzi.

Elliptic na kampuni zingine kama Chainalysis zinaweza kufuatilia pesa zilizoibiwa kama Bitcoin na Ethereum kwa kufuatilia orodha ya miamala.

Kwa miaka mingi watafiti wamegundua mfanano wa mbinu na zana zinazopendwa na wadukuzi wa Korea Kaskazini.

Pamoja na udukuzi wa ByBit mwezi Februari, wachambuzi wa Elliptic wamehusisha zaidi ya mashambulizi mengine 30 ya Korea Kaskazini kufikia sasa mwaka huu.

Wizi wa mwaka huu umevunja rekodi ya wizi mkubwa zaidi wa mwaka 2022 wa jumla ya dola bilioni 1.35.

Papa kuzuru nchi zenye Waislamu wengi mwezi Novemba

dc
Maelezo ya picha,Papa Leo akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa siku tatu “Kuinua Tumaini kwa masuala ya Hali ya Hewa” huko Castel Gandolfo, karibu na Roma, Italia, Oktoba 1, 2025.

Katika safari yake ya kwanza nje ya nchi, Papa Leo atasafiri kwenda Uturuki na Lebanon mwishoni mwa Novemba, Vatikani imetangaza siku ya Jumanne.

Papa Leo ni kiongozi mpya wa wa Kanisa Katoliki duniani lenye waumini bilioni 1.4.

Leo, Papa wa kwanza wa Marekani, atazuru Uturuki kuanzia Novemba 27-30 kabla ya kuelekea Lebanon kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 2, ambako anatarajiwa kuzungumza kuhusu masaibu ya Wakristo katika Mashariki ya Kati na kutoa wito wa amani katika eneo lote.

Shughuli za serikali ya Marekani kuendelea kufungwa

tg

Seneti ya Marekani imeshindwa kwa mara ya tano siku ya Jumatatu kupitisha hatua za ufadhili ambazo zingeifungua tena serikali.

Mapendekezo ya chama cha Democratics na Republican yote yalipigwa chini, na kushindwa kufikia kiwango cha kura 60 kinachohitajika.

Donald Trump amerudia vitisho vya kuwaachisha watu kazi, kwa wingi ikiwa kura hiyo itashindwa.

Maelfu ya wafanyakazi wa serikali ya shirikisho wamesitishwa kufanya kazi au kuamriwa kufanya kazi bila malipo wakati ufadhili wa mashirika yao ulipomalizika siku tano zilizopita.

Rais wa Marekani amedokeza kwamba yuko tayari kumaliza mzozo huo na ikiwezekana atafanya makubaliano na Democratic ambao wanashikilia matakwa ya kutaka sheria ya kushughulikia huduma za afya. Warepublican wanashinikiza kupitishwa kwa mswada wa ufadhili uliopo sasa.

Mswada unaoongozwa na Democratis wa kuongeza ufadhili wa serikali ulishindwa Jumatatu kwa kura 45-50. Muswada wa chama cha Republican ulishindwa kwa kura 52-42.

Democratics hawaungi mkono pendekezo linaloongozwa na Republican kwa sababu wanasema linapunguza upatikanaji wa huduma za matibabu kwa Wamarekani wa kipato cha chini.

Wanataka mswada wowote wa ufadhili kuhakikisha ruzuku ya bima ya afya kwa Wamarekani wa kipato cha chini haumalizikiwi na muda na kuondoa punguzo la utawala wa Trump kwa mpango wa afya wa Medicaid.

Warepublican wamewashutumu mara kwa mara Democrats kwa kuifunga serikali ili kuendeleza huduma za afya kwa wahamiaji wasio na vibali – jambo ambalo viongozi wa Democratic wanakanusha.

Jaji apigwa risasi na kuuawa mahakamani

y
Maelezo ya picha,Tukio hilo lilitokea wakati wa kusikilizwa kesi katika Mahakama ya Rufaa ya Tirana siku ya Jumatatu

Jaji mmoja nchini Albania ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya mtu mmoja kufyatua risasi wakati wa kesi katika Mahakama ya Rufaa katika mji mkuu wa Tirana.

Jaji Astrit Kalaja alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini, maafisa walisema, huku wengine wawili waliohusika katika ya mzozo wa mali – baba na mwana – walipigwa risasi lakini walipata majeraha ambayo hayakuwa hatari kwa maisha.

Polisi wamesema walimkamata mshukiwa wa kiume mwenye umri wa miaka 30.

Waziri Mkuu wa Albania Edi Rama ametoa rambirambi zake kwa familia ya Jaji Kalaja Pia ametaka ulinzi mkali ndani ya mahakama za nchi hiyo na adhabu kali kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Mshukiwa wa mauaji ya Jaji Kalaja alifyatua risasi kwa sababu alitarajia kushindwa katika kesi hiyo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya eneo hilo.

Mjomba wa mtuhimiwa ni mlinzi wa mahakama, pia ameripotiwa kukamatwa kutokana na tukio hilo.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Albania Olsian Çela alisema kufuatia tukio hilo kwamba usalama wa majaji unahitaji kuimarishwa “katika kila jambo.”

Kutekwa kwa Polepole: Polisi yaanzisha uchunguzi

KJMN

Jeshi la polisi nchini Tanzania limeanzisha rasmi uchunguzi wa tuhuma za kutekwa kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kama zilivyotolewa na familia yake.

Hata hivyo katika taarifa hiyo wameongeza kuwa wanamtafuta ndugu wa Humphrey Polepole, aitwaye Augustino Polepole kuthibitisha tuhuma hizo.

”Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili aweze kutupa ushirikiano na kutoa maelezo yake ya uthibitisho wa shutuma alizotoa kwamba afisa wa jeshi la Polisi alihusika katika tukio alilolitolea taarifa katika mitandao ya kijami,’’ inaeleza taarifa ya Polisi.

Aidha Jeshi hilo limesema linataka uthibitisho kuwa Humphrey Polepole alikuwa mkazi wa nyumba inayodaiwa utekaji kutendeka.

Humphrey Polepole alijiuzulu nafasi ya ubalozi na kuvuliwa rasmi hadhi ya ubalozi kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi wake na Rais Samia Suluhu Hassan.

Uamuzi wake ulifuatia kile alichoeleza kutoridhishwa na mwenendo wa mambo mbalimbali nchini Tanzania akidai hawezi kuwa sehemu ya serikali isiyojali misingi ya haki, sheria na katiba ya nchi.

Waziri Mkuu wa Uingereza awataka wanafunzi kutoandamana tarehe 7 Oktoba

Sir Keir

Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer amewataka wanafunzi wasijiunge na maandamano yanayounga mkono Wapalestina siku ya Jumanne, ikiwa ni mwaka wa pili tangu shambulio la Oktoba 7 la Hamas dhidi ya Israeli, akionya “kuongezeka kwa chuki mitaani kwetu”.

Sir Keir alisema “sio ustaarabu wa Waingereza” kufanya maandamano katika maadhimisho hayo ambayo, alisema, yametumiwa na baadhi ya watu kama “kisingizio cha kudharauliwa kuwashambulia Wayahudi wa Uingereza”.

Uingereza imeshuhudia usalama ukiiimarishwa kulinda jamii za Wayahudi, kufuatia shambulio baya la wiki iliyopita kwenye sinagogi mjini Manchester.

Wanafunzi kutoka vyuo vya London wanapanga maandamano ya pamoja katika mji mkuu, huku Manchester, Glasgow, Edinburgh, Bristol na Sheffield ni miongoni mwa miji mingine inayosemekana kutarajia maandamano.

Vyuo vikuu vya Uingereza, ambavyo vinawakilisha sekta ya vyuo vikuu, vilisema wakati vyuo vikuu vilikuwa mahali ambapo maoni tata yanaweza kutolewa, wanafunzi na wafanyakazi wanaoshiriki katika maandamano wanapaswa kuzingatia wakati wa maandamano yaliyopangwa kufanyika tarehe 7 Oktoba.

Sir Keir alisema kwamba wakati baadhi wamepinga hatua za serikali ya Israel huko Gaza, “wengine wametumia hili kama kisingizio cha kuchukiza kuwashambulia Wayahudi wa Uingereza kwa jambo ambalo hawana jukumu lolote”.

Sir Keir alisisitiza kwamba Uingereza “daima itasimama na kuungana” dhidi ya wale wanaotaka kudhuru jamii za Kiyahudi. “Jumuiya zetu za Kiyahudi pia zimevumilia kuongezeka kwa chuki katika mitaa yetu, katika nchi yetu,” aliongeza.

Shirika la Umoja wa Mataifa lasema karibu 80% ya miundombinu ya Gaza iliharibiwa tangu kuanza kwa vita

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina limesema zaidi ya wafanyakazi 370 wa Gaza wameuawa tangu kuanza kwa vita.

Ikiadhimisha miaka miwili tangu shambulio lililoongozwa na Hamas Oktoba 7 na kampeni kubwa ya kijeshi ambayo Israel ilianzisha baada ya matokeo yake, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina (Unrwa) limetoa takwimu zinazoeleza ukubwa wa uharibifu huo.

Hizi ni baadhi ya takwimu muhimu za shirika la Umoja wa Mataifa:

Zaidi ya watu 66,100 waliripotiwa kuuawa, wakiwemo watoto wasiopungua 18,430.

Hadi watu milioni moja wamejihifadhi katika vituo vya Unrwa, takribani 845 kati yao waliuawa walipokuwa wakijihifadhi.

Zaidi ya wafanyikazi 370 wa Unrwa wameuawa.

Takriban 80% ya miundo mbinu katika ukanda mzima imeharibiwa.

Chini ya 40% ya hospitali zinasalia kufanya kazi, kwa kiasi cha Takriban 90% ya mali za maji na usafi wa mazingira zimeharibiwa.

Rais wa Madagascar amteua Jenerali wa jeshi kuwa waziri mkuu mpya

Jenerali wa jeshi Ruphin Fortunat Zafisambo
Maelezo ya picha,Jenerali wa jeshi Ruphin Fortunat Zafisambo

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amemteua Jenerali wa jeshi Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa waziri mkuu siku ya Jumatatu, wiki moja baada ya kuivunja serikali kutokana na maandamano yanayoendelea kuhusu uhaba wa umeme na maji.

Zafisambo alichukua nafasi ya Waziri Mkuu Christian Ntsay, ambaye alifutwa kazi kama sehemu ya hatua ya rais.

Jenerali huyo alikuwa mkurugenzi wa baraza la mawaziri la kijeshi katika ofisi ya waziri mkuu hadi uteuzi huu.

Kabla ya kumtaja, Rajoelina alisema nchi hiyo inahitaji “waziri mkuu mwenye uwezo wa kurejesha utulivu na imani ya watu.”

Rais alitangaza uteuzi huo wakati wa hafla ya moja kwa moja iliyopeperushwa kwenye ukurasa wake wa Facebook na runinga ya serikali.

Hii ni wiki ya pili ya maandamano katika nchi ya visiwa vya Bahari ya Hindi, ambapo vijana wanadai uwajibikaji wa serikali kwa huduma duni muhimu za umma.

Mnamo Jumatatu ya wiki jana, Rajoelina alivunja serikali yake kama njia ya kujibu hasira ya wanarika wa Gen Z, lakini hatua hiyo haikuweza kuwatuliza waandamanaji.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu wasiopungua 22 wamepoteza maisha na zaidi ya 100 kujeruhiwa katika machafuko hayo.

Vifaa vya Uingereza vilipatikana katika ndege zisizo na rubani za Urusi, Zelensky asema

Zelensky

Kompyuta ndogo za Uingereza zilikuwa miongoni mwa zaidi ya bidhaa 100,000 zilizotengenezwa na wageni zilizokuwa kwenye makombora na ndege zisizo na rubani za Urusi zilizotumika katika mashambulizi ya Jumapili dhidi ya Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema.

Rais wa Ukraine alitoa wito wa vikwazo zaidi baada ya kusema sehemu zinazotoka katika nchi washirika zikiwemo Ujerumani, Japan na Marekani zimetambuliwa katika silaha za Urusi.

Wizara ya Biashara (DBT) ilisema hivi karibuni imefanya jitihada za kukabiliana na makampuni ya Uingereza ambayo bidhaa zao zimeendelea kuingia katika mlolongo wa usambazaji wa kijeshi wa Urusi.

“Tunachukua ripoti za bidhaa kutoka kwa makampuni ya Uingereza kupatikana katika silaha za Kirusi kwa uzito mkubwa,” msemaji wa serikali alisema.

Msemaji huyo alisema serikali “imepiga marufuku usafirishaji wa maelfu ya bidhaa kwenda Urusi ikiwa ni pamoja na za uwanja wa vita ambao Ukraine imeleta kwetu,” na kuongeza kwamba wameweka “vikwazo vikali zaidi”.

Mama wa mateka wa Israel anasema bado hajui kama kijana wake yu hai au amekufa

Herut Nimrodi anasema anashikilia kutumaini kwamba mwanawe Tamir "bado ananing'inia" miaka miwili baada ya kutekwa nyara.
Maelezo ya picha,Herut Nimrodi anasema anashikilia kutumaini kwamba mwanawe Tamir “bado ananing’inia” miaka miwili baada ya kutekwa nyara.

Mama wa mwanamume wa Israel aliyetekwa na Hamas tarehe 7 Oktoba 2023 anasema bado hajui kama mtoto wake amekufa au yu hai, lakini ana “matumaini ya kweli” kwamba mpango wa amani wa Rais wa Marekani Donald Trump utawarudisha mateka wote walioshikiliwa Gaza.

Herut Nimrodi aliambia BBC kwamba “anahofia mabaya zaidi” kwa mwanawe Tamir, mwanajeshi asiye wa vita, lakini alikuwa akishikilia matumaini kwamba “bado anaendelea kushikilia” miaka miwili baada ya kutekwa nyara.

Alisema alikuwa mateka pekee wa Israel ambaye familia yake haikuambiwa kama walikuwa hai au wamekufa.

Mpango wa amani uliopendekezwa na Trump umekuwa ukishika kasi, huku mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yakitarajiwa kuendelea Jumanne kati ya Hamas na Israel ili kumaliza vita na kuwarudisha mateka.

“Wamekuwa wakijaribu kuunda makubaliano kwa muda lakini hayakuanza. Wakati huu inahisi tofauti,” Bi Nimrodi alisema. “Kuna matumaini ya kweli kwamba hii ndiyo, hii ni mpango wa mwisho.”

Alisema ilikuwa muhimu sana kwamba mateka wote – walio hai na waliokufa – wataachiliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo.

“Hii ni kubwa, hii ni baraka kwetu,” alisema. “Ni haraka kuwaachilia mateka – wale ambao bado wako hai, na hata wale ambao wamefariki. Hatujui miili yao iko katika hali gani. Inabidi tuwaachie ili familia ziwe na aina fulani ya kufungwa. Hata familia zilizopata ujumbe kwamba wapendwa wao wamekufa, hazikubali kwa sababu zinahitaji ushahidi.”

Tamir ni mmoja wa mateka 47 waliotekwa nyara tarehe 7 Oktoba ambao wamesalia Gaza – 20 kati yao wanaaminika kuwa bado hai.

Maaskofu wa Katoliki DRC wapinga hukumu ya kifo dhidi ya Joseph Kabila,

Joseph Kabila

Baraza la Maaskofu wa Kitaifa wa Congo (CENCO) limelaani hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Rais wa zamani Joseph Kabila na Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Kinshasa.

Wakielezea imani hiyo kuwa haipatani na maadili ya Injili, maaskofu wanadai kwamba mantiki ya kuadhibu ya hukumu ya kifo inashindwa kukuza amani au mshikamano wa kitaifa.

Badala yake, wanasisitiza mazungumzo jumuishi ili kushughulikia mizozo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakisema, “mazungumzo jumuishi yanasalia kuwa njia bora ya kushughulikia vyanzo vya migogoro hii na kurejesha umoja na amani.

Pia walitoa wito wa juhudi za pamoja za kukataa hukumu ya kifo na kuweka kipaumbele katika ujenzi wa amani ili kuhakikisha uadilifu wa eneo na ustawi wa watu wa Congo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CENCO; Monsinyo Donatien Nshole Jumatatu, ilitiwa saini na Askofu Mkuu Fulgence Muteba, Rais wa CENCO.

Kabila alihukumiwa kifo bila kuwepo mahakamani kwa uhalifu wa kivita na uhaini tarehe 30 Septemba 2025.

Mashtaka hayo yanahusu shutuma kwamba Kabila amekuwa akiunga mkono kundi la M23, kundi la waasi ambalo limesababisha uharibifu katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa zamani aliitaja kesi hiyo kama “holela” na akasema mahakama zilikuwa zinatumiwa kama “chombo cha ukandamizaji”.

Fifa yaishutumu Malaysia kwa kughushi utaifa wa wachezaji waliozaliwa nje

y
Maelezo ya picha,Wachezaji saba wazaliwa wa kigeni katika timu ya taifa ya kandanda ya Malaysia, wamesimamishwa

Fifa inaishutumu nchi ya Malaysia kwa kughushi nyaraka za uraia ili wachezaji saba waliozaliwa nje ya nchi hiyo wacheze katika timu ya taifa.

Shirikisho hilo la soka duniani limepiga faini na kuwafungia wachezaji hao mwishoni mwa Septemba, na siku ya Jumatatu ilitoa ripoti ya kuhalalisha hatua yake.

Fifa imesema Shirikisho la Soka la Malaysia (FAM) limeghushi vyeti vya kuzaliwa ili ionekane babu na bibi wa wachezaji hao walizaliwa Malaysia.

Fifa imesema, “hiyo ni aina ya udanganyifu.”

Lakini FAM imesema hitilafu hizo zilitokana na “kosa la kiutawala” na itakata rufaa dhidi ya adhabu za Fifa. Ikishikilia kuwa wachezaji hao ni “raia halali wa Malaysia.”

Sheria ya Fifa inaruhusu wachezaji wa mpira wazaliwa wa nchi za kigeni kuwakilisha nchi ambazo wazazi wao wa kibaiolojia au babu na bibi walizaliwa.

Sheria hiyo inalenga kuzuia timu za kandanda kuchukua tu wachezaji wa kigeni ili kuongeza ubora wa timu.

Fifa iliwachunguza wachezaji hao kufuatia ushindi wa Malaysia wa 4-0 dhidi ya Vietnam mwezi Juni.

Mwezi Septemba, kamati ya nidhamu ya Fifa iliwafungia wachezaji saba kwa mwaka mmoja na kuwaamuru kulipa faini ya faranga 2,000 za Uswizi ($2,500; £1,870). Wakati huo, Fifa haikutoa maelezo kuhusu sababu ya kusimamishwa kwao.

Fifa imeiamuru FAM kulipa faranga 350,000 za Uswizi ($440,000; £330,000).

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment