Matatizo Yanayoweza Angamiza ndoto Yako.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Robbie Montgomery mwanamama kutoka Missisipi alikuwa na ndoto kubwa ya kuwa Muimbaji…

Alifanya bidii na mazoezi na akafanikiwa kuwa mwimbaji kama “Back Vocal” katika timu ya waimbaji ya Joe Cocker…

Baadaye Tina Turner na Stevie Wonder.

Hata hivyo baada ya muda aligundulika na tatizo na Mapafu lililomfanya ashindwe kuendelea na uimbaji.

Akajiuliza jambo gani lingine analoweza kulifanya vizuri kwenye maisha yake…

…na akagundua ni kupika; Jambo ambalo lilitokana na ukweli kuwa alikuwa ni mtoto wa kwanza katika watoto 9 wa familia.

Na kila wakati alipokuwa nyumbani wazazi wake walikuwa wanampa kazi ya kuandaa chalula kwa ajili ya wadogo zake.

Alipobadilisha mwelekeo na kutoka kuimba na kuanza kupika kibiashara alianza kupata mafanikio Makubwa sana…

…hadi kufanikiwa kuwa na kipindi katika Program za Television ya Oprah Winfrey Network (OWN).

Kuna mambo kwenye maisha yanaweza kutokea na kukatisha safari ya Ndoto yako.

Badala ya Kukaa Pembeni na kuanza kulalamika na kunung’unika

“Jiulize ni Kitu gani kingine naweza kufanya kwa sasa?”.

Usikubali chochote kinachotokea kwenye maisha yako kikufanye uone “Hauwezi kufanya Kitu chochote cha maana”.

Unaweza kuamua kuandika stori yako kwa Upya (Re-write your own story).

Leo unapoanza siku usikubali chochote kile kikuzuie kuchukua hatua Mpya…

…hata kama mlango uliokuwa unautarajia umefungwa.

TAFUTA NAMNA NYINGINE.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment