Ninakumbuka maisha yangu ya safari ya utafutaji nilipitia changamoto nyingi
kipindi hicho nilikuwa natafuta pakulala mjini,baada ya kutoka vijijini ni safari ndefu,Mungu alinipa ndugu wengi chuoni nilipokua nasomea uanahabari.
Wakati chakula kilikua ni tatizo kwangu lakini sikukata tamaa.
Ilikuwa siku ya ijumaa nilikuwa kipindi hicho kwa mjomba yangu, waliniambia wanahamia mtaa wa Langata hivyo nitafute sehemu nyingine pakukaa.
Nilijihisi kama nipo yatima maana sikuwa napakwenda, nilikumbuka ,nikakumbuka watu waliofanikiwa wana mengi waliyopitia mazito sana,nikajipa moyo hata mimi siku yangu inakuja.
Hivyo nikaadhimia moyoni mwangu kuto kumwambia mtu yoyote hali yangu ninayopitia nikamwomba Mungu anipe mahali pakukaa, na niliwaaga kule bila kuwaambia, week inayofuata nitaondoka. “Niliwadanganya nahamia hostel za chuo ili wasiniulize maswali na wasiwe na wasiwasi ninavyoondoka”🙈🙈
Nilijisemea moyoni kama Mungu asipo fungua njia basi nitaenda kwa rafiki zangu pale chuo niombe waniwekee vitu vyangu na mabegi kulala nitaenda kulala kwenye madarasa, tena nilijisemea nitajifanya
Siku ya jumapili ilipofika nilikuwa na sh 500/= tuu, nakumbuka nikasema nibora nitembee kwa mguu kwenda kanisani umbali kama km 4 hivi, maana sikuwa na nauli ili hiyo 500/= iwe sadaka.Nilipenda kwenda kwa mchungaji Pius Muiru kupokea mafundisho yaliniweka mjini nikiwa mwanafunzi kipindi hicho.
Mungu wewe unanijua vyema, wajua moyoni mwangu kuna nini, wajua ninachowaza akilini mwangu, hivyo Mungu naomba kesho
Unipe sh. 20,000/= (nilijisemesha tuu)
Jumatatu yake ndo ilikuwa siku mtihani unaanza, nakumbuka nilikuwa sina hata kalamu, nikajaribu kukopa hata 2,000 kwa kila mtu nikakosa, nikaona nikama milango yote imefungwa kwangu, kila nikijaribu kuomba msaada sipati.
Wazazi wangu waliniombea na kuchakarika na kunipa kila nafasi ya kufaulu,walijitolea ili nifikie ndoto zangu.Mungu anajibu maombi.
Kuanzia siku hiyo nikajifunza kumtegemea Mungu kama Baba na mzazi wa kwanza kwangu.
Leo hii ninapotazama yale Mungu ametenda ninatokwa na machozi,ni ushuhuda
Kwenye kuomba vitu vikubwa vikubwa nilijifunza, na ndipo nilipoanza kuweka list ya maombi na mahitaji kwenye diary. Na kuweka tiki kwenye Yale yanayopata majibu..
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.