Papa Leo atoa wito wa kufanikisha mpango wa amani huko Gaza

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo amesema ana matarajio kuwa mpango wa hivi karibuni wa kumaliza vita huko Gaza utapata matokeo yanayotarajiwa.

Vatikan | Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIVPicha: Filippo Monteforte/AFP

Na:Cantona Joseph|RFA

Akizungumza wakati wa sala ya kila wiki, Papa amezitaka pande zote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa amani, akisisitiza hitaji la haraka la kuumaliza mzozo huo na kuanzisha “amani ya haki na ya kudumu”.

Wapatanishi wa Israel na Hamas wamekutana Jumapili mjini Cairo katika mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo huo wa  Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema Israel na Hamas zimekubaliana kuhusu sehemu kubwa ya mpango huo wa amani uliopendekezwa na rais Donald Trump lakini akasisitiza kuwa suala la kundi hilo kupokonywa silaha ndio linalojadiliwa kwa sasa na linatarajiwa kuleta utata.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment