Naongea na mtu ambae kibiashara umeanguka,kiuchumi umeanguka, kimasomo umeanguka, ki mahusiano umeanguka, na kihuduma umeanguka
Na inawezekana kabisa umezungukwa na watu wanaokucheka na kukudharau maana wanafikili mwisho wako ndo huo, nikiwa katika maombi Bwana akaniambia waambie kuna kuinuka tena
Ndipo Bwana akanipa neno hili na akaniambia wape na wakilipokea kwa imani hata kama kila kitu kimeanguka na kuteketea kitainuka tena
Ayubu 22:29
Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena;Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa.
Ninakuombea kwa imani ukainuke tena mbele yao waliokuangusha na kukucheka,waliofikili ndio mwisho wako,waliofikili safari yako imeishia hapo
Nimekuombea ukainuke tena katika jina la Yesu inategemea imani yako lakini ninaona wale watakaolipokea neno hili kwa imani,ninaona wakiinuka tena,
Ki elimu ukainuke tena, ki huduma ukainuke tena, ki uchumi ukainuke tena, kimahusiano na kibiashara ukainuke tena na katika kila eneo la maisha yako ukainuke katika jina la Yesu.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.