Wajumbe wa Israeli na Hamas wanajiandaa kwa mazungumzo Misri

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wajumbe wa Israeli na Hamas wanajiandaa kwa mazungumzo ya Misri, huku matumaini ya kusitishwa mapigano Gaza yakiongezeka baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kusema huenda kutakuwa na tangazo la kuachiliwa kwa mateka

Na:Cantona Joseph|RFA

Khalil al-Hayya, afisa wa ngazi ya juu wa Hamas ambaye amewakilisha kundi la wanamgambo wa Kipalestina katika mazungumzo ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana mateka, akizungumza wakati wa mahojiano na The Associated Press, mjini Istanbul, Uturuki, Aprili 24, 2024.

Kesho Jumanne itakuwa inatimia miaka miwili tangu shambulio la Hamas lililoanzisha vita. Rais wa Marekani Donald Trump amepongeza tamko la Hamas linalokubali baadhi ya vipengele vya mpango wa amani wa Marekani. Israel imesema inaunga mkono juhudi mpya za Marekani. Kwa mujibu wa mpango huo, Hamas itawaachilia mateka 48 waliobaki, ikiwa takriban 20 wanaaminika kuwa hai ndani ya siku tatu. Pia itakubali kuachia madaraka na kusalimisha silaha. Kwa mujibu wa ofisi ya Netanyahu, ujumbe wa Israel unaoongozwa na mpatanishi mkuu Ron Dermer leo hii unatarajiwa kuwasili Sharm el-Sheikh kwa mazungumzo hayo. Na duru kutoka  Misri zinasema ujumbe wa Hamas tayari umefika.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment