Mashambulizi matatu tofauti ya anga yashambulia Gaza asubuhi ya leo

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jeshi la Israeli limesema kuwa usalama wa wanajeshi wake ni kipaumbele cha juu na kuonya “hatua za haraka zitachukuliwa kukabiliana na tishio lolote” linaloweza kutokea.

Na:Cantona Joseph|RFA

  1. Wizara ya Afya ya Palestina – Gaza inasema takriban watu 66 wameuawa na uvamizi wa Israel katika saa 24 zilizopita, na kuongeza idadi ya waliouawa katika Ukanda huo tangu 7 Oktoba hadi 67,074. Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema watu wengine 265 waliojeruhiwa wamefika katika hospitali za Ukanda wa Gaza katika muda huo huo. Wizara hiyo inasema imekuwa vigumu kufikia watu ambao wamenaswa chini ya vifusi.
  2. Ni nini kimekuwa kimetokea Gaza leo? Milipuko kadhaa imeshuhudiwa huko Gaza mapema Jumamosi, huku mji wa Gaza ukikumbwa na mashambulio matatu tofauti ya anga, na kuua mtu mmoja, saa chache baada ya Trump kuitaka Israeli kuacha kushambulia Ukanda huo.IDF imewaonya Wapalestina kwamba kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na karibu na Mji wa Gaza bado ni “eneo hatari la mapigano”, na kuwataka tena watu kuhamia kusini.Viongozi wa upinzani wameunga mkono mpango wa amani wa Trump na kumtaka Netanyahu kuunga mkono mpango huo.Mshirikishe mwenzako, Takriban watu 66 wauawa Gaza katika saa 24 zilizopita – Hamas.

Mazungumzo ya amani kuanza tena nchini Misri

.

Mazungumzo ya makubaliano kati ya Israel na Hamas yanatarajiwa kurejelewa nchini Misri katika siku zijazo, baada ya kundi hilo kukubali kuwaachilia mateka wote waliosalia, lakini limesema linataka mazungumzo zaidi kuhusu masuala mengine.

Hamas ilikuwa chini ya shinikizo kubwa la kukubali angalau baadhi ya vipengele vya mpango wa Trump kwa Gaza, na hivi ndivyo walivyofanya.

Lakini mambo muhimu bado hayajaafikiwa, ikiwa ni pamoja na kundi hilo kuachana na silaha, sharti ili wanajeshi wa Israel waondoke Gaza na hakikisho la kwamba Israel haitaanzisha tena vita baada ya mateka kuachiliwa.

Katika mji wa Gaza, kumekuwa na mashambulizi ya anga licha ya wito wa Trump kwa Israel wa kusitisha mapigano katika eneo hilo.

Rais Trump amehusika kibinafsi katika mazungumzo hayo, na anatoa shinikizo kwa vita hivyo kumalizika. Hatua kubwa imepigwa katika mpango wa Trump – lakini hii sio hakikisho kwamba makubaliano yamefikiwa.

Mashambulizi matatu tofauti ya anga yashambulia Gaza asubuhi ya leo

.

Mji wa Gaza umekumbwa na mashambulio matatu tofauti ya anga tangu saa za asubuhi, moja likiwa limeua mtu mmoja na kuwaacha wengine kadhaa kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya matibabu katika hospitali ya al-Shifa.

Shambulizi la kwanza lililenga kundi la wakaazi karibu na Shule ya al-Nasr mtaani al-Nasr walipokuwa wakijaribu kuangalia nyumba zao. Lilitekelezwa na helikopta ya Israeli.

Shamblizi la pili lilishambulia Mtaa wa al-Jalaa, kati ya maeneo ya Zaharna na Ghafri, ingawa hakuna majeruhi walioripotiwa. Shambulizi la tatu la anga lilifanywa na ndege za kivita za Israel karibu na mzunguko wa Hamid, kwenye makutano ya barabara ya al-Nasr.

Maelezo ya majeruhi au uharibifu bado hayajawekwa wazi.

Wakati huo huo, magari na ndege zisizo na rubani za Israel (quadcopters) zimeendelea kurusha makombora na kushambulia majengo katika maeneo ambayo jeshi linafanya kazi.

Mutharika wa Malawi aapishwa kwa muhula wa pili kama rais

.

Peter Mutharika wa Malawi ameapa kumaliza ufisadi serikalini na kujenga upya uchumi uliodorora baada ya kuapishwa Jumamosi kwa muhula wa pili kama rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Mutharika, 85, alipata zaidi ya 56% ya kura mwezi uliopita, na kumshinda rais anayemaliza muda wake Lazarus Chakwera, 70, aliyepata 33% ya kura zilizopigwa.

Wapiga kura walimkataa Chakwera baada ya miaka mitano ya mgogoro wa kiuchumi unaozidi kuwa mbaya katika mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani.

Katika hotuba yake ya kuapishwa, alisema utawala wake unarithi nchi iliyo katika msukosuko wa kiuchumi.

Malawi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, gharama ya juu ya maisha, na ukosefu wa fedha za kigeni ambao umedumaza biashara na kusababisha uhaba wa mafuta, alisema.

“Hakuna pesa serikalini. Kukopa ni kiwango cha juu sana, na hakuna anayejua pesa zilizokopwa zimeenda wapi,” alisema.

Lakini aliahidi maboresho, akisema: “Tutaiweka sawa nchi hii.

Takriban watu 30 wajeruhiwa katika shambulizi la Urusi kwenye kituo cha reli, Zelensky asema

.

Takriban watu 30 wamejeruhiwa kufuatia shambulizi la ndege zisizo na rubani za Urusi kwenye kituo cha reli kaskazini-mashariki mwa Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymy Zelensky amesema.

Katika chapisho kwenye mtandao wa X, alisema kuwa ripoti za awali zilionyesha wafanyakazi wa treni na abiria walikuwa kwenye eneo la tukio katika jiji la Shostka, eneo la Sumy.

Huduma za dharura zinatolewa katika eneo la tukio na kusaidia watu, alisema na kuongeza kuwa taarifa kuhusu majeruhi bado zinakusanywa.

Pia alichapisha video inayoonyesha behewa la treni lililoharibika likiwaka moto.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment