Jina la mshambuliaji wa sinagogi la Manchester latangazwa, tukio lililoelezwa kuwa “ugaidi”

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Polisi wanashuku huenda mshambuliaji huyo alitayarisha bomu kwa ajili ya matumizi katika shambulio hilo.

Na:Cantona Joseph|RFA

Polisi wa Uingereza wametangaza kuwa wamemtambua mhusika wa shambulio hilo lililotoka Alhamisi asubuhi ndani ya sinagogi katika eneo la Crumpsall, kaskazini mwa Manchester.

Shambulizi hilo lililosadifiana na Yom Kippur, siku takatifu zaidi katika kalenda ya Kiyahudi, lilisababisha vifo vya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa, akiwemo mlinzi, kwa mujibu wa Polisi.

Polisi wa Uingereza walisema mshambuliaji huyo aliyetambulika kwa jina la Jihad al-Shami, Muingereza mwenye umri wa miaka 35 mwenye asili ya Syria, aliendesha gari lake hadi kwa wapita njia nje ya Sinagogi ya Usharika wa Heaton Park Hebrew kabla ya kuwashambulia kwa kisu. Aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika eneo la tukio.

Polisi walitangaza kukamatwa kwa watu wengine watatu kama sehemu ya uchunguzi, na kuelezea tukio hilo kama “tukio la kigaidi.”

Kulingana na polisi, walipokea ripoti saa 9:31 asubuhi kwa saa za huko kuhusu gari lililowagonga waumini nje ya sinagogi, kabla ya mtu mmoja kuendelea kuwachoma visu kadhaa.

Dame Sarah Mullally ateulia mwanamke wa kwanza kuwa Askofu Mkuu wa Canterbury

Mully

Kwa mara ya kwanza katika karibu miaka 500 ya historia, Kanisa la Anglikana limemteua mwanamke kuliongoza.

Dame Sarah Mullally, 63, ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu Mteule wa Canterbury.

Alikuwa akijenga msingi mpya katika taaluma yake aliyoichagua hata kabla ya kuwa kasisi.

Mwaka wa 1999 akawa afisa mkuu wa uuguzi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea nchini Uingereza.

Kwa zaidi ya miaka saba amehudumu kama Askofu wa London, mshiriki mkuu wa tatu wa makasisi katika Kanisa na mwanamke wa kwanza kufanya kazi hiyo.

Wanawake wameruhusiwa tu kuwa mapadre katika Kanisa la Anglikana tangu katikati ya miaka ya 1990.

Lakini kuna maaskofu wakuu katika Kanisa la Anglikana ambao wanapinga waziwazi wanawake kujiunga na ukasisi hata kidogo kuongoza taasisi hiyo.

Sheria inawahitaji Maaskofu Wakuu wa Canterbury kustaafu wakiwa na umri wa miaka 70, ambayo labda ni sababu mojawapo kwa nini wengine hawakumwona Dame Sarah Mullally akiwa na nafasi ya kuchaguliwa.

Hata hivyo ameishia kuandikisha historia. Tarehe ya kutawazwa kwakerasmi bado haijatangazwa.

Mtoto wa Robert Mugabe afikishwa mahakamani kwa tuhuma za dawa za kulevya

.

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefikishwa katika mahakama ya Harare akikabiliwa na shtaka la kupatikana na dawa za kulevya.

Robert Mugabe Jr, 33, alikamatwa Jumatano asubuhi alipokuwa akiendesha gari kwa njia isiyo sahihi katika barabara ya njia moja, kulingana na hati za mahakama.

Polisi walipekua begi jeusi alilokuwa amevaa wakati huo na inadaiwa walipata sacheti mbili ndogo za bangi.

Kufuatia tukio hilo, polisi walisema katika taarifa kwamba watu watano “waliohusishwa naye” pia walikamatwa.

Wakili wa Bw Mugabe aliambia BBC wanapanga kukana mashtaka, na kupinga madai yaliyotolewa na polisi.

Bw Mugabe aliyekuwa amevaa kofia nyekundu huku akiwa anazungumza na simu yake alipokuwa akiongozwa kwenda katika mahakama ya hakimu siku ya Alhamisi. Alizungukwa na watu na hakuwa amefungwa pingu.

Mahakama ilimweka rumande Bw Mugabe akisubiri uamuzi wa dhamana siku ya Ijumaa.

Polisi wamesema wataendelea na uchunguzi.

Putin aonya Marekani dhidi ya kupeleka makombora Ukraine

.

Rais wa Urusi Vladimir Putin Alhamisi ameonya kwamba kupeleka makombora ya Marekani ya Tomahawk nchini Ukraine kutasababisha “kiwango kipya cha mashambulizi”, pamoja na kuharibu uhusiano kati ya Urusi na Marekani.

Akizungumza katika mkutano huko Sochi, Putin alisema hilo halibadilisha hali ilivyo katika mstari wa vita, ambako Urusi inafikia maendeleo yake ingawa kwa mwendo wa taratibu inasonga mbele.

“Utumiaji wa makombora ya Tomahawk bila uwepo wa jeshi la Marekani ni jambo lisilowezekana. Hii itasababisha kiwango kipya kabisa cha mashambulizi, pamoja na uhusiano wa Urusi na Marekani, Putin alisema.

Kiongozi huyo wa Urusi alisema kuwa hata kama makombora ya Tomahawk yatasababisha uharibifu kwa Urusi ikiwa yatapelekwa Ukraine, ulinzi wa anga wa Urusi utaitikia haraka tishio jipya.

Misri inajitahidi kushawishi Hamas kukubali mpango wa Trump, asema waziri wa mambo ya nje

.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema Alhamisi kwamba nchi yake inashirikiana na Qatar na Uturuki kuwashawishi Hamas kukubali mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kumaliza vita vilivyodumu takriban miaka miwili huko Gaza, na kuonya kwamba mzozo huo utaongezeka ikiwa kundi la wanamgambo litakataa.

Akizungumza katika Taasisi ya Uhusiano ya Kimataifa ya Ufaransa mjini Paris, Badr Abdelatty amesema ni wazi kuwa Hamas inabidi iweke silaha chini na Israel isipewe kisingizio cha kuendelea na mashambulizi yake huko Gaza.

“Tusitoe kisingizio chochote kwa upande mmoja kutumia Hamas kama kisingizio cha mauaji haya ya kichaa ya kila siku ya raia. Kinachotokea ni zaidi ya kilichofanyika tarehe saba ya Oktoba,” alisema, akimaanisha shambulio la Hamas la 2023 dhidi ya Israeli, ambapo watu 1,200 waliuawa na zaidi ya watu 200 walichukuliwa mateka, kulingana na Israeli.

Mashambulizi ya Israel yameua zaidi ya watu 66,000 huko Gaza, mamlaka ya afya ya Palestina inasema.

“Ni zaidi ya kulipiza kisasi. Haya ni mauaji ya kikabila na kimbari. Kwa hiyo inatosha,” Abdelatty alisema.

Ikulu ya White House ilitoa mapema wiki hii mpango wenye vipengele 20 ambao ulitaka kusitishwa kwa mapigano mara moja, kubadilishana mateka wanaoshikiliwa na Hamas kwa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel, hatua ya Israel ya kujiondoa kutoka Gaza, upokonyaji silaha wa Hamas na serikali ya mpito inayoongozwa na chombo cha kimataifa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment