Wanaharakati 2 wa Kenya watekwa nyara nchini Uganda walipokuwa kwenye kampeni ya Bobi Wine

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wanaharakati wawili wa nchini Kenya, Bob Njagi na Nicholas Oyoo, wameripotiwa kutekwa nyara nchini Uganda katika mazingira ya kutatanisha. 

Robert Kyagulanyi, anayejulikana pia kama Bobi Wine, wa chama cha National Unity Platform (NUP) akionyesha ishara kwa wafuasi wake alipokuwa akiwasili kwa mkutano baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais, katika kitongoji cha Nateete jijini Kampala, Uganda Septemba 24, 2025. REUTERS/Abubaker Lubowa
Robert Kyagulanyi, anayejulikana pia kama Bobi Wine, wa chama cha National Unity Platform (NUP) akionyesha ishara kwa wafuasi wake alipokuwa akiwasili kwa mkutano baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais, katika kitongoji cha Nateete jijini Kampala, Uganda Septemba 24, 2025. REUTERS/Abubaker Lubowa © Abubaker Lubowa / REUTERS

Wawili hao  inasemekana walitekwa na watu wanne waliokuwa wamejihami kwa bunduki na walioaminika kuwa maofisa wa usalama, ambapo waliingizwa kwa nguvu kwenye gari na baadae simu zao kuzimwa.

Rafiki aliyenusurika, amesema tukio hilo linahusishwa na wawili hao kumuunga mkono Bobi Wine, ambapo wakati wakikamatwa walikuwa sehemu ya msafara wa kampeni wa mwanasiasa huyo.

Video zilizorekodiwa wakati wa kampeni ya  Bobi Wine katika wilaya ya Kamuli mashariki mwa Uganda, zinaonesha Bob Njagi ambaye ni kiongozi wa Free Kenya Movement akiwa jukwani na Bobi Wine.

Utekaji huo unajiri miezi minne kupita tangu mwanaharakati wa Kenya Bonface Mwangi na mwenzake wa Uganda  Agather Atuhaire watekwe nyara nchini Tanzania  na kisha kutupwa katika mipaka ya nchi zao ambapo baadae walidai kuteswa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ikiwemo vile vya kingono.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment