HADITHI YA MJASIRIAMALI ALIYEPAMBANA.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Siku moja nilikutana na kijana aitwaye Yusuf, kutokea Mombasa Kenya. Alinihadithia maisha yake, alisema….Alipomaliza shule hakuwa na ajira, lakini alikuwa na ndoto kubwa ya kumiliki biashara yake. Hakuwa na mtaji mkubwa, bali alianza kuuza karanga na maji barabarani.

Watu wengi walimdharau na kumcheka, wengine wakamwambia kuwa…

“Wewe huwezi kufanikiwa kwa kuuza vitu vidogo kama hivi.”

Lakini Yusuf hakuacha. Kila siku alijiwekea akiba kidogo kutoka kwenye faida yake. Badala ya kutumia hela yote, alihesabu, akaandika, na akahifadhi.

Baada ya miezi kadhaa, akaweza kufungua kibanda kidogo cha kuuza vinywaji na vitafunwa jijini Mombasa. Alijifunza mbinu za kuhudumia wateja vizuri na akawa tofauti na wengine. Wateja walimpenda kwa sababu ya uaminifu na huduma yake bora.

Mwaka uliofuata, Yusuf alikuza biashara yake na kufungua duka kubwa zaidi. Leo hii, ameajiri vijana kadhaa na anasambaza bidhaa zake kwenye maduka makubwa ya rejareja.

Yusuf alisema…

“Nilianza na kidogo, nilichokuwa nacho si mtaji mkubwa, bali nidhamu na uvumilivu. Siri ya mafanikio yangu ni kutokata tamaa.”

Mafunzo kutoka kwenye hadithi hii..

1. Usidharau mwanzo mdogo.

Wengi hadi sasa hawaajanzisha biashara wanasema hawana mtaji, ila kumbe kile walichonacho kingeweza kuwafikisha mbali sana.

2. Akiba na nidhamu ni mtaji wa kweli.

Tabia ya kuweka akiba ni mbegu ya mafanikio makubwa.

3. Huduma bora kwa wateja hujenga brand yako.

Mteja ukiweza kumhudhumia vizuri atakuwa ni barozi kwa watu wengine.

4. Changamoto ni za muda, mafanikio ni ya kudumu kwa wenye kusimama imara.

Unahitaji kuwa na uvumilivu mkubwa katika biashara kwani mabadiliko na kupata ni uhakika.

Umejifunza nini katika kisa hiki.?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment