Mahakama yatupilia mbali pingamizi ya mawakili wa utetezi katika kesi ya Machar

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama maalumu nchini Sudan Kusini inayosikiliza kesi ya uhaini, mauaji na dhulma za kibinadamu dhidi ya aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, imetupilia mbali pingamizi la mawakili wa utetezi waliodai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo.

Makamu wa Rais nchini Sudan Kusini.
Makamu wa Rais nchini Sudan Kusini. AP – Denis Farrell

Mahakama hiyo inayoongozwa na jaji James Alala, ikitupilia mbali madai ya Machar, imesema hana kinga ya kutoshtakiwa, ikiamuru kesi hiyo kurejelewa kuanzia hapo kesho.

Mawakili wa Machar, walikuwa wanapinga kesi hiyo kuskilizwa na mahakama hiyo kwa kile walidai ni kesi ya kisiasa.

Aidha Machar alitaka kesi yake kusikilizwa na mahakama  maalum ya Umoja wa Afrika kwa mujibu wa mkataba wa amani wa 2018  uliomaliza vita vya wenyewe.

Tuhuma dhidi ya Machar zimetokana na waasi waliofanya mashambulizi mwezi Machi katika eneo la White Nile na kuwauwa wanajeshi 250 akiwemo jenerali wa jeshi la Sudan, kesi hii ikiibua wasiwasi kuhusu nchi hiyo kurejea kwenye vita.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment