Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Denmark imepiga marufuku ndege zote zisizo na rubani wiki hii kabla ya kongamano la Umoja wa Ulaya ambalo litafanyika njini Copenhagen, waziri wa uchukuzi wa nchi hiyo alitangaza Jumapili.
Wazara hiyo ilisema hatua hitua hiyo ilifikiwa ili “kurahisisha shughuli za usalama” kwa polisi, na kwamba hawataruhusu “droni za kigeni kuibua hali ya taharuki”.
Denmark ni mojawapo wa mataifa kadhaa za Ulaya zilizoripoti “visa vya droni kuingia anga zao bila idhini” katika wiki za hivi karibuni, tukio la hivi punde likiwa la moja ya droni hizo zikipaa juu ya kambi yake ya kijeshi ya siku ya Jumamosi.
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 10 za Umoja wa Ulaya wamekubali kuunda “ukuta wa ulinzi wa ndege zisizo na rubani” ili kukabiliana na matukio hayo, na Nato inasema “imeimarisha ulinzi” katika eneo lote la Baltic.
Marufuku hiyo itadumishwa hadi tarehe 3 Oktoba, na yule atakayekiuka atakabiliwa na faini au kifungo cha hadi miaka miwili.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.