Ushelisheli kuandaa duru ya pili ya uchaguzi wa urais

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Duru ya pili itafanyika kuanzia tarehe 9-11 Oktoba
Maelezo ya picha,Duru ya pili itafanyika kuanzia tarehe 9-11 Oktoba

Ushelisheli inatarajiwa kufanya marudio ya uchaguzi wake wa urais kati ya wagombea wawili wakuu, baada ya kukosekana kwa mshindi wa moja kwa moja.

Kiongozi wa upinzani Patrick Herminie alipata 48.8% ya kura dhidi ya Rais aliyeko madarakani Wavel Ramkalawan ambaye alipata 46.4%, tume ya uchaguzi ilitangaza.

Kulingana na kanuni za uchaguzi, mgombea lazima apate zaidi ya 50% ya kura ili kutangazwa mshindi.

Duru ya pili ya uchaguzi huo sasa umeratibiwa kufanyika wiki ijayo.

Ushelisheli ni nchi ndogo zaidi barani Afrika katika Bahari ya Hindi na idadi ya zaidi ya watu 120,000.

Wagombea wanane waliwania urais katika uchaguzi uliofanyika wa wiki iliyopita.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment