Wakenya waliojikuta katika vita nchini Urusi waokolewa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Serikali ya Kenya inasema ujumbe wake huko Urusi umeokoa na kuwarudisha raia watatu ambao walisafirishwa kwenda nchini humo.

Hili linawadia wiki moja baada ya Wizara ya Mambo ya nje kusema ilikuwa inafuatilia ripoti za Wakenya kadhaa zinazodai walilazimishwa kuingia kwenye jeshi la Urusi na baadaye kutekwa kama wafungwa wa vita huko Ukraine.

Katika taarifa kwenye vyombo vya habari vya kijamii, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje nchini Kenya Korir Sing’oei alisema wanaume wawili na mwanamke mmoja wako salama na wanarudi nyumbani kwa familia zao.

Tangazo hilo linafuatia operesheni ya usalama jijini Nairobi mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo viongozi waligundua kile wanachoamini kuwa ni kikundi cha usafirishaji watu kilichowashawishi raia na ahadi za kazi zenye faida kubwa huko Moscow lakini baada ya kuwasili wakajikuta wamelazimishwa kuingia katika jeshi la Urusi na kupelekwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya Ukraine.

Kesi hiyo imevutia nadhari baada ya jeshi la Ukraine kutoa video ya mwanariadha wa Kenya, ambaye alisema alidanganywa kujiunga na jeshi la Urusi na aliomba kurudishwa nyumbani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment